MARAIS WATANO WA MAREKANI WAMESHINDWA KUMUONDOA RAIS WA IRAN, TRUMP ATAWEZA?!!!...

Fahamu kwa nini Marekani haijafanikiwa kumuangusha Ayatollah Ali Khamenei Mpaka Sasa. Kuanzia mwaka 1989 mpaka sasa mwaka 2026 Marais tofauti tofauti wametoa matamko Mengi ya vitisho ila mwamba Khamenei bado Anadunda tena kwa jeuri kabisa.
Ifahamike Marais wote hawa wimbo wao ni mmoja Kumpiga Khamenei tu.
Picha unayo iona hapa ni Mfululizo wa marais wa Marekani kwa miaka tofauti kuanzia mwaka 1989 hadi πŸ‘‰ 2021 - 2026.
Chini kabisa ni Kiongozi Mkuu wa Iran yani Supreme Leader akipeperusha mkono kwa Madaha ya kejeli.
Marais wote hawa walishindwa kumuangusha mtu huyu HakikaπŸ‘‰ Marekani ni dhaifu dhidi ya uongozi wa Iran.
Kwa nini Marekani haijafanikiwa kumuondoa Ayatollah Ali Khamenei?
Hii ndio hoja ya msingiπŸ‘‰ Khamenei si Rais Bali Khamenei ni mfumo.
Tofauti na Saddam au Gaddafi.
Khamenei Yuko juu ya
πŸ‘‰Serikali
πŸ‘‰Yuko juu ya jeshi
πŸ‘‰Yuko juu ya mahakama
πŸ‘‰Yuko juu ya vyombo vya habari
πŸ‘‰Yuko juu ya uchumi wa kimkakati
πŸ‘‰Yeye ni Dola ndani ya Dola
Mbali na kua Mfumo ila ufisadi kwake ni laana hajioni Mungu mtu wala hamuonei mtu, Hachokozi Nchi yoyote.
Hata ukimuua Rais wa Iran πŸ‘‰ Khamenei na mfumo wake unabaki.
Ana jeshi lake binafsi πŸ‘‰IRGC
Ayatollah Khamenei anadhibiti vikosi vya kijeshi kama
πŸ‘‰IRGC Revolutionary Guards
πŸ‘‰Quds Force
πŸ‘‰Intelligence
πŸ‘‰Makombora
πŸ‘‰Drones
Pamoja na πŸ‘‰Mtandao wa Hezbollah, Houthis, Syria, Iraq
Hili ni jeshi linalomtii yeye binafsi, si serikali.
Marekani ikitaka vita na Iran haitapigana na mtu mmoja itapigana na mtandao wa kimataifa wa kivita.
Iran si nchi ya Kuivamia Rahisi Rahisi, Iraq ilikuwa rahisi kuvamiwa kwasababu
πŸ‘‰Hakukuwa na milima
πŸ‘‰Hakukuwa na jeshi la kiitikadi
πŸ‘‰Hakukuwa na makombora ya masafa marefu
Iran ina
πŸ‘‰Milima mikubwa
πŸ‘‰Wananchi waliokomaa kwenye vita
πŸ‘‰Maelfu ya makombora
πŸ‘‰Mamilioni ya wanamgambo wa kieneo
Kuivamia Iran ni sawa na kuanzisha Vita kubwa zaidi ya WWII
Kumuondoa Khamenei kunamaanisha Marekani inajua
Akifa Khamenei kwa shambulio, πŸ‘‰ Iran itarusha maelfu ya makombora kwa
πŸ‘‰Israel
πŸ‘‰Gulf
πŸ‘‰US bases
πŸ‘‰mafuta ya dunia
Hiyo inaweza kusababisha
πŸ‘‰Bei ya mafuta kupanda
πŸ‘‰Vita ya kikanda
πŸ‘‰Kushiriki kwa China na Russia
Ndiyo maana Marekani wanatumia πŸ‘‰ vikwazo
πŸ‘‰ vita ya kiuchumi
πŸ‘‰ vita ya kisaikolojia
πŸ‘‰ propaganda
πŸ‘‰ mitandao ya kijamii
πŸ‘‰ maandamano
Lakini si uvamizi wa moja kwa moja ni kitu hatari sana.
Picha unayoiona ina msingi wa ukweli huu
πŸ‘‰Marekani Inashindwa kumuondoa Khamenei kwa sababu gharama ya kufanya hivyo ni kubwa kuliko faida.
Ni kwamba kumshinda Khamenei kungegharimu dunia nzima.
Marais wote hawa wa Marekani wamechemka kumudondosha mwamba Khamenei
1) George H. W. Bush
πŸ‘‰1989 – 1993
2) Bill Clinton
πŸ‘‰1993 – 2001
3) George W. Bush
πŸ‘‰2001 – 2009
4) Barack Obama
πŸ‘‰2009 – 2017
5) Donald J. Trump
πŸ‘‰2017 – 2021 Mpaka sasa.
Baki na Mimi kwa Mengi zaidi yanayo jiri Duniani
By Professor Chotara Mweusi Sultan kutoka viunga vya πŸ‘‡
πŸ‘‰Sharif shamba
πŸ‘‰Ilala Dar es salaam
πŸ‘‰Tanzania
Bingwa la uchambuzi wa maswala ya kijamii, Uchumi na Siasa za Dunia Yetu.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MAPACHA WATATU FAMILIA YA MWAIKENDA WAPATA KIPAIMARA

MVUA KUBWA KUNYESHA MIKOA 20

AINA 4 ZA WANAWAKE WASIOWEZA KUDUMISHA NDOA.

MIKOA 10 YENYE KIPATO KIKUBWA ZAIDI KWA MTU MMOJA MMOJA

IJUE HISTORIA YA MCHEZAJI MZUNGU WA TANZANIA