MIKOPO YA ELIMU YA JUU HUTOLEWA BILA KUJALI MWANAFUNZI KATOKA SHULE ZA SERIKALI AU BINAFSI - WANU

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir amefafanua kwamba Upangaji na utoaji mikopo ya Elimu ya Juu unaongozwa na Sheria ya Bodi ya Mikopo (SURA 178) ambayo inabainisha sifa za msingi za mwombaji zikiwepo sifa za kitaaluma za kujiunga na Taasisi za Elimu ya Juu kwa waombaji waliothibitika kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama za Elimu ya Juu. "Serikali inaendelea kutoa mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu wanaotoka katika kaya maskini bila kujali mwombaji ametoka shule za Serikali au shule binafsi. Kwa msingi huo, Serikali kupitia Bodi ya Mikopo imeweka utaratibu wa kuzingatiwa kwa waombaji wote bila kujali shule aliyosoma mwombaji ilimradi mwombaji amekidhi vigezo vilivyowekwa ikiwemo ujazaji wa taarifa sahihi." Naibu Waziri Wanu ametoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Devotha Daniel aliyeihoji wizara hiyo kwamba Serikali haioni umuhimu wa kurekebisha kigezo kinachowapunguzia fursa Wanafunzi wa Shule Binafsi kupata Mikopo ya Elimu ya Juu?



IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MIKOA 10 YENYE KIPATO KIKUBWA ZAIDI KWA MTU MMOJA MMOJA

BODABODA ALIPWA PIKIPIKI BAADA KUSAFIRI KWA BODA KWA SAA 10 MBEYA HADI DAR

ASANTE GWIJI YAYA TOURE KWA KUPASUA UKWELI UKWELI KUPENDELEWA KWA MOROCCO

AINA 4 ZA WANAWAKE WASIOWEZA KUDUMISHA NDOA.

CONFIRMED HAWA NDIO WACHEZAJI WETU 12 WA KIGENI 🦾