Miaka 1000,kama siyo kocha Pedro Yanga wasingempata DEPU.
Kwenye hili dili Yanga wametumia zaidi ya bilion 1.2 ya Tanzania (pesa ya kimununua na pesa binafsi ya mchezaji) Guys haikuwa Rahisi hata kidogo Yanga kufika huko,haya mambo wanafanya Al ahly,Mamelodi na vilabu vya Uarabuni.
Kabla ya kwenda Ulaya,Depu alikuwa mchezaji bora x2 wa COSAFA,pia alikataa ofa ya Al ahly Cairo, Orlando Pirates na Kaizer Chiefs.
Kwa miaka miwili Depu amecheza kwenye ligi tatu ngumu π
πLigi ya Γreno dhidi ya timu za FC Porto,Lisbon na Benfica.
π Ligi ya Serbia dhidi ya timu ngumu na kubwa kama Crvena zvezda na Partizan.
π Ligi ya Poland,dhidi ya timu kubwa kama Lech PoznaΕ,Jagiellonia BiaΕystok na Legia Warszawa.
Hizo timu zote tatu alizocheza DEPU ni kubwa na zinafanya vizuri kwenye Ligi husika.
Pale Ureno,amecheza Gil Vicente,ambao wako nafasi ya nne nyuma ya Porto,Lisbon na Benfica.
Pale Serbia klabu Yake ya FK Vojvodina,iko nafasi ya tatu Nyuma ya Partizan na Crvena zvezda.
Halafu pale Poland,klabu Yake ya Radomiak iko nafasi ya saba,kwenye Ligi yenye timu kumi na nane.
Sitaki kusema Kama atafanya poa sana Bongo Ila nataka niwambushe ukubwa wake na sehemu alikotoka.
Depu ni mchezaji mkubwa na mkali sana,anaweza kuipeleka mbali Yanga kwenye michuano ya CAF.

Comments