Bajeti ya Mwaka 2025/2026
(tarehe 1.7.2025 - 30.6.2026)
Ukubwa wa Jimbo:
Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374
(i) Miundombinu ya Umeme Vijijini:
Vijiji vyote 68 vina miundombinu ya umeme (Mafanikio - Ngazi ya Vijiji: 100%)
(ii) Vitongoji vilivyokwisha unganishiwa umeme:
(a) Bajeti ya Mwaka 2025/2026
Vitongoji 46 +4:
Maana ya 46+4 - Usambazaji utafanywa kwenye Vitongoji 46 na Vitongoji 4 vitaongezwa (ombi la Mbunge limekubalika REA) ili kufikia Vitongoji 50
Kiambatanisho: Vitongoji 46
Wakandarasi wameishapatikana na kazi za usambazaji umeme zimeaanza kwenye Vitongoji 46 +4
(b) Vimesalia Vitongiji 50 kati ya 374:
Miradi ya Bajeti ya Mwaka 2025/2026 ikikamilika Jimbo letu litakuwa limebakiza Vitongozi 50 tu kukamilisha usambazaji wa umeme ndani ya Vitongoji vyetu 374
Mafanikio - Ngazi ya Vitongoji: 86.6%
(iii) Umemejua (solar) Visiwani:
Wakandarasi wamepatika na kazi ya kusambaza umemejua (solar) kwenye VISIWA VYETU VYOTE itaanza hivi karibuni
Kiambatanisho: Orodha ya Visiwa vyenye miradi ya umemejua (solar)
Taarifa ya miradi ya umeme ya Jimboni mwetu imetolewa na REA.
Shukrani:
Wananchi na Viongozi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kuishukuru Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kugharamia miradi ya maendeleo ya Jimboni mwetu.
REA inapewa pongezi nyingi mno kwa kazi nzuri na umahiri wake wa kusambaza umeme Jimboni mwetu.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe: 15 Jan 2026


Comments