WENYEVITI WAPYA WA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE HAWA HAPA

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamefanya uchaguzi wa viongozi wa kamati za kudumu za bunge, kulingana na maelekezo ya kanuni za bunge namba 138 (1), za mwaka 2025.

Majina ya washindi wa uchaguzi huo ni : Anne Kilango Malecela, Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, makamu wake ni Christina Solomon Mndeme.

Subira Hamis Mgalu - Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, ambapo makamu wake ni Simon Songe Lusengekile.

Dkt. Johannes Lembulung Lukumay - Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Masuala ya Ukimwi, huku makamu wake akiwa ni Zeyana Abdallah Hamid.

Cecilia Paresso - Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ndogo na Yahaya Mfaume Zuberi, amechaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa kamati hiyo.

Ado Shaibu - Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na makamu wake ni Abdallah Dadi Chikota.

Devotha Minja - Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na makamu wake ni Khalfan Hilaly Aeshi.

Masanja Kadogosa - Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) na makamu wake Dougras Massaburi.

Mashimba Ndaki - Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti na makamu wake ni Ally Hassan Omar King.

Kamati ya Miundombinu - Moshi Seleman Kakoso na makamu wake ni Abubakari Damian Asenga.

Timotheo Mnzava - Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii na makamu wake ni Mary Masanja.

Husna Sekiboko - Mwenyekiti Kamati ya Elimu, Utamaduni na Michezo akisaidiwa na makamu wake Cornel Magembe.

Kamati ya Maji na Mazingira ni Jackson Kiswaga na makamu wake ni Profesa Pius Yanda.

Kamati ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii - Hawa Mchafu na msaidizi wake ni Regina Malima.

Kamati ya TAMISEMI, inaongozwa na Florent Kyombo na makamu wake ni Jafari Chage.

Najma Giga, anaongoza Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama akisaidiwa na Paschal Chinyele.

Kamati ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo - Deodatus Mwanyika na makamu wake ni Mariam Mzuzuri.

Dkt. Damas Ndumbaro, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Utawala, Katiba na Sheria na msaidizi wake ni Edwin Enosy Swale.

Bunge hilo linarejea katika kikao cha pili, Januari 27, mwaka huu.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MAPACHA WATATU FAMILIA YA MWAIKENDA WAPATA KIPAIMARA

MVUA KUBWA KUNYESHA MIKOA 20

AINA 4 ZA WANAWAKE WASIOWEZA KUDUMISHA NDOA.

MIKOA 10 YENYE KIPATO KIKUBWA ZAIDI KWA MTU MMOJA MMOJA

IJUE HISTORIA YA MCHEZAJI MZUNGU WA TANZANIA