MARUFUKU WATUMISHI WA UMMA KUTUMIA MIFUMO ISIYO RASMI KUWEKA NYARAKA ZA SERIKALI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete akifunga Kikao kazi cha 6 cha Serikali mtandao kilichafanyika kwa siku Tatu Mkoani Arusha.

 

Serikali imepiga marufuku watumishi wa Uma Kutumia mitandao isiyo rasmi ambayo ni tofauti na ile iliyounganishwa na mfumo wa Serikali mtandao katika kutuma nyaraka na taarifa mbalimbali za serikali kwani si salama kwa usalama wa nchi na wananchi

 Marufuku hiyo imetolewa  l9 April 2026  na Waziri wa Nchi, Ofisi ya   Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete wakati akifunga kikao kazi cha 6 cha serikali mtandao kilichofanyika kwa siku Tatu mkoani Arusha nakusema kwamba  watumishi wa Umma kutumia mifumo isiyo rasmi ni hatari kwani inasababisha nyaraka za siri za serikali kuonekana mtandaoni. 

Bado tunao wafanyakazi wa Serikali wanatumia Mtandao binafsi kurusha taarifa za Serikali jambo ambalo siyo sawa kwa taarifa hizo za Serikali kuwekwa wazi jambo hilo liwe narufuku kuanzia Leo taarifa za Serikali kutumwa kwa Mtandao binafsi. Alisema

Kikao Kazi hicho  cha siku tatu, kimewakutanisha takribani washiriki 1,000 kutoka sekta za umma na binafsi, na kimejadili kwa kina masuala muhimu yanayohusu ujenzi, uendelezaji na usimamizi wa jitihada za Serikali Mtandao. Ambapo Kupitia mijadala hiyo wamepata fursa ya: Kutathmini utekelezaji wa maazimio ya Kikao Kazi kilichopita,, Kubainisha mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa miradi ya TEHAMA Serikalini,

Pia waliweza Kujadili changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana nazo,Na kuweka maazimio mapya yatakayotuongoza katika hatua zinazofuata za kuendelea kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma za umma kwa njia ya kidijitali.

Kikwete amesema amefarijika kuona kuwa, mijadala yote imejikita katika uzingatiaji wa Sheria, Kanuni,Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao, jambo ambalo ni msingi muhimu wa kuhakikisha miradi ya TEHAMA Serikalini inakuwa salama, endelevu na yenye kujali Katika kikao kazi hiki, 

Sambamba na hayo Serikali kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), itatoa tuzo kwa taasisi zilizofanya vizuri katika kuzingatia Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao, kwenye utekelezajiwa miradi ya TEHAMA.ambapo  amezipongeza taasisi zote zilizotunukiwa tuzo hizo  na kusema Tuzo hizo si za heshima tu, bali ni chachu ya kuhamasisha ubora, uwajibikaji na uzingatiaji wa misingi ya Serikali Mtandao katika taasisi zote za umma.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Wasifu wa Kizza Besigye

KILA MWANAMKE ANAPASWA KUFAHAMU HII...

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

MAMBO MADOGO YANAYOVUTIA KWA MPENZI WAKO

DKT. MAJULE AKABIDHIWA CHETI CHA SHUKRANI UWT DODOMA KUFANIKISHA USHINDI WA CCM 2025

UWT YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI YA RUFAA DODOMA

30 TANZANIAN PROJECTS IN THE NEXT 10 YEARS

TRC YAANZA RASMI USAFIRISHAJI WA MIZIGO KWA KUTUMIA CONTAINER CARRIERS SGR