Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw.
Bakari Machumu akizungumza na Waandishi wa Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam
tarehe 16 Februari, 2026 kuhusu Ziara za Kikazi za Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alizofanya Jijini Addis Ababa
nchini Ethiopia tarehe 12-15 Februari, 2026 pamoja na Dubai, Umoja wa Falme za
Kiarabu (UAE) tarehe 2-6 Februari, 2026.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Kundo
Mathew akizungumza katika Mkutano wa Waandishi wa Habari, Ikulu Jijini Dar es
Salaam kuhusu Ziara ya Kikazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyofanya Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe
12-15 Februari, 2026. Naibu Waziri Mhandisi Kundo alizungumzia kwa kina masuala
mbalimbali yaliyojiri kwenye sekta ya maji pamoja na faida ambazo Tanzania
imepata katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Biashara ya
Kimataifa na Diplomasia ya Uchumi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi John Ulanga akizungumza katika Mkutano wa
Waandishi wa Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam kuhusu Ziara ya Kikazi ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyofanya
Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) tarehe 2-6 Februari, 2026. Mhe. Balozi John Ulanga alielezea fursa
mbalimbali ambazo Tanzania imepata kupitia Uwekezaji wa Teknolojia ya
Mawasiliano.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria Mkutano wa
Waandishi wa Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Februari, 2026 kuhusu
Ziara za Kikazi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan, alizofanya Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 12-15
Februari, 2026 pamoja na Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) tarehe 2-6
Februari, 2026.


.jpeg)
.jpeg)





Comments