TUTAPIGA MAKAZI YA TRUMP MWENYEYWE" Iran 🇮🇷 Yaonya.

Mwananchama wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge la Iran Mheshimiwa Said Hayat Mughaddam ameonya kuwa Hakuna Mahala ambako Makombora ya Kimkakati ya Iran yatashindwa kufika ikiwa Nchi hiyo itachokozwa. 


"Ndiyo, Hawazijui Silaha zetu, lakini Ni kweli kabisa Hakuna sehemu ambako Silaha zetu za kujihami, kushambulia, za Kimkakati zitashindwa kufika"... 

" Kwa sasa Hata MAKAZI binasfi ya Rais Trump hayako salama. Tunaweza kuyasambaratisha... Na ninadhani hiyo ndiyo itakuwa njia fupi zaidi ya kumtia Adabu Adui " Ni kwa vile Iran tumekuwa wema tu, hatumvamii Mtu, wala hatuanzishi Vita na Taifa geni, kamwe tumebakia Watu wa Amani na Wapenda Amani kuliko Taifa lolote mashariki ya kati"... Alisema Bwana Mughaddam, Ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Iran. 

Mwezi Juni mwaka 2025, Benjamin Netanyahu waziri mkuu wa Israel wakati anaomba msaada kwa Marekani, alipata kuonya kuwa Makombora ya Iran yamevuka mipaka ya Mashambulizi, akimuonya Rais wa Marekani kuwa Hali iliyokuwa inaendelea haitaishia Tel Aviv pekee. 

"Ni vema Mheshimiwa Rais Trump akajua, Iran imevuka mipaka, Hali hii haitaishia hapa, Leo ni Tel Aviv, lakini Kesho itakuwa Washington, ama New York, hii ni hakika... Nami nasema"... Bwana Netanyahu alisisitiza...



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Wasifu wa Kizza Besigye

KILA MWANAMKE ANAPASWA KUFAHAMU HII...

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

MAMBO MADOGO YANAYOVUTIA KWA MPENZI WAKO

DKT. MAJULE AKABIDHIWA CHETI CHA SHUKRANI UWT DODOMA KUFANIKISHA USHINDI WA CCM 2025

UWT YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI YA RUFAA DODOMA

30 TANZANIAN PROJECTS IN THE NEXT 10 YEARS

TRC YAANZA RASMI USAFIRISHAJI WA MIZIGO KWA KUTUMIA CONTAINER CARRIERS SGR