VETA KUENDESHA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KUPITIA SIMU JANJA

ILI kuwapa vijana na wananchi wengine uhuru zaidi wa kujifunza mafunzo ya, ufundi stadi popote walipo na kwa muda wao, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeanzisha mfumo uitwao VSOMO unaomwezesha mwanafunzi kujifunza maarifa yote ya ufundi stadi kwa kutumia simu ya mkononi, kufanya mtihani kwenye simu hadi mwisho wa mpango wa mafunzo ya nadharia.

Mfumo huo umeelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kwenye Ukumbi wa Wizara ya Habari, Mji Serikali Mtumba jijini Dodoma Februari16, 2026, kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa siku 100 wa ahadi zilizotolewa na Rais Samia alipoapishwa Novemba 3, 2025.

Baada ya hapo, atapangiwa kufanya mafunzo ya vitendo kwenye chuo kimojawapo cha VETA. Hii inapunguza muda wa kukaa chuoni na inaongeza matumizi bora ya simu za mkononi na muda wa mafunzo. Vilevile, mpango huu unawapa fursa watu walio mbali na vyuo kupata mafunzo ya ufundi stadi,”amesema  CPA Masore.

“VSOMO ilikuwa ikitekelezwa kwa ushirikiano wa VETA, Airtel na Kampuni ya Magilla Tech. Hata hivyo, mwaka jana, VETA ilikabidhiwa rasmi mfumo huu ambapo kwa sasa VSOMO inapatikana kupitia mitandao yote ya simu iliyopo nchini. “

Ametaja stadi zipatazo ishirini (20) zinazotolewa kupitia mfumo wa VSOMO, kuwa ni; Ufundi wa Pikipiki; Ufundi wa Umeme;  Ufundi wa Aluminium na PVC; Umeme wa Magari; Utandazaji na Ufungaji Mabomba; Utengenezaji wa Kompyuta; Upishi na Utoaji Huduma ya Chakula (Catering); Uokaji Mikate na Upambaji; Usafi wa Majengo Makubwa na Maeneo ya Umma; Maua na Upambaji kwenye Shughuli; Ujasiriamali; Utengenezaji wa Simu za Mkononi; Ufungaji Mabomba Viwandani; Umeme wa Viwandani; Uungaji Vyuma Viwandani na Urembo.

Mpaka sasa Takribani wanafunzi 533 wamemaliza kozi mbalimbali kupitia mfumo huu wa VSOMO na kutunikiwa vyeti.

Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Antony Masore.
Wanahabari wakisikiliza kwa makini katika mkutano huo.

Baadhi ya viongozi wa Idara ya Habari MAELEZO na VETA wakiwa katika mkutano huo.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, Kelvin Kanje akihitimisha mkutano huo.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

ASANTE GWIJI YAYA TOURE KWA KUPASUA UKWELI UKWELI KUPENDELEWA KWA MOROCCO

Wasifu wa Kizza Besigye

CONFIRMED HAWA NDIO WACHEZAJI WETU 12 WA KIGENI 🦾

KILA MWANAMKE ANAPASWA KUFAHAMU HII...

RAIS WA SENEGAL AWAPATIA ZAWADI NONO WACHEZAJI WALIOFANIKISHA UBINGWA WA AFCON 2025

NYOMI YA WASENEGALI WAKISHANGILIA UBINGWA WA AFCON 2025

TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA FIFA

CCM YAMJIBU BUTIKU CHADEMA KUFUNGIWA

MAMBO MADOGO YANAYOVUTIA KWA MPENZI WAKO