Yeye hakutawala nchi tu aligeuka kuwa hiyo nchi.
Jina lake alikuwa Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga — jina alilojipa mwenyewe likimaanisha: "Shujaa mwenye nguvu zote ambaye, kwa sababu ya uvumilivu wake na utashi usioyumba wa kushinda, huenda kutoka ushindi mmoja hadi mwingine, akiacha moto nyuma yake."
Hata jina lake tu lilikuwa kama ikulu.
Wakati viongozi wengi wa Afrika miaka ya 1970 walikuwa wakikopa pesa kutoka IMF ili tu kuweka serikali zao hai... Mobutu alikuwa akiagiza Concorde — ndege ya abiria ya gharama kubwa zaidi kuwahi kutengenezwa duniani — ili imletee mikate ya Croissants freshi kutoka Paris hadi kwenye ikulu yake iliyopo katikati ya msitu.
Si mkate wa kawaida. Si chakula kwa ajili ya watu wake wanaokufa njaa.
Ni Croissants. Kutoka Paris. Kwa kutumia Concorde.
Ikulu yake ya Gbadolite — iliyojengwa ndani kabisa ya msitu wa mvua wa Congo — ilikuwa na sakafu za marumaru (marble) zilizoagizwa kutoka Ulaya, barabara ya ndege (runway) ndefu ya kutosha kutua ndege ya kijasusi ya mwendo wa kasi, na taa za thamani (chandeliers) ambazo zingemfanya mfalme wa Ufaransa, Versailles, apate wivu.
Wafalme wa Ulaya walikuwa na majumba yaliyojengwa kwa karne nyingi kwa jasho la maelfu ya watu. Mobutu alijenga yake kwa miaka michache — akitumia pesa zilizoibiwa kutoka kwa moja ya mataifa tajiri zaidi duniani.
Congo imekalia utajiri wa madini wenye thamani ya Dola Trilioni 24. Kobalti. Koltani. Dhahabu. Almasi. Malighafi ambazo zinawasha simu yako unayotumia sasa hivi.
Simu yako. Imetengenezwa na udongo wa Congo. Na Mobutu alihakikisha hakuna mkulima hata mmoja wa Kikongo aliyeona hata dola moja ya utajiri huo.
Alimiliki majumba ya kifahari (châteaus) nchini Uswisi, nyumba za kifahari (villas) kule French Riviera, na ikulu nchini Ureno. Utajiri wake binafsi ulipofika kileleni ulikadiriwa kufikia Dola Bilioni 5 — kiasi ambacho kilikuwa sawa na deni lote la taifa la Zaire wakati huo.
Soma hapo tena.
Mtu mmoja. Utajiri mmoja. Sawa na deni la nchi nzima.
Na mataifa ya Magharibi — Marekani, Ubelgiji, Ufaransa — walijua. Walimpa ruzuku, walimpa silaha, walimpa mkono na kutabasamu mbele ya kamera. Kwa sababu wakati wa Vita Baridi, kiongozi fisadi wa Afrika alikuwa na faida kwao kuliko Waafrika walio huru.
Alivaa kofia yake ya ngozi ya chui kila mahali — alama, aliyosema, ya uhalisia wa Mwafrika (African Authenticity). Alipiga marufuku suti na majina ya Kimagharibi. Aliiita "Authenticité" — kurejea kwenye utambulisho wa Kiafrika.
Lakini mvinyo wake (champagne) ulikuwa wa Kifaransa.
Wasanifu majengo wake walikuwa Wabelgiji.
Madaktari wake walikuwa Waswisi.
Pesa zake zilikuwa kwenye benki za Ulaya.
"Mwafrika halisi" zaidi katika historia... aliishi maisha ya Kizungu kuliko hata Wazungu wenyewe.
Alipoanguka hatimaye mwaka 1997, ikulu yake iliporwa ndani ya saa chache.
Taa za thamani — zilichukuliwa.
Marumaru — zimenyolewa.
Barabara ya ndege — ilimezwa na msitu.
Asili haifanyi mazungumzo na wafalme.
NB: Hata huko Malawi wapo wakina Mobutu wengi sana na wanajinufaisha kwa rasilimali za nchi, huku wenye nchi wakijazana darasa moja watoto mia moja.
Follow page yangu kwa makala nyingine na stori na chambuzi murua.

Comments