MAJANI YA MAPERA NA MATUMIZI YAKE YA KITIBA


Majani ya mpera yana faida nyingi za kiafya, lakini watu wengi hawajui thamani yake kubwa ya kitabibu. Yana vitamini A, B, na C, potasiamu, nyuzinyuzi (fiber), lycopene, quercetin, catechin na virutubisho vingine muhimu.

Hapa chini ni baadhi ya faida zake:
▪️Afya ya Ubongo
Vitamini B6 na B3 husaidia kuboresha mzunguko wa damu kwenda kwenye ubongo, kuongeza uwezo wa kufikiri, na kutuliza mishipa ya fahamu.

▪️Huongeza Kinga ya Mwili
Chai ya majani ya mpera huimarisha kinga na kusaidia kupunguza hatari ya magonjwa mbalimbali.

▪️Kupunguza Maumivu
Quercetin husaidia kupunguza maumivu na kupambana na maambukizi.

▪️Msaada wa Hedhi
Inaweza kusaidia kupunguza maumivu ya hedhi, kurekebisha mzunguko, na kupunguza usumbufu.

▪️Ngozi Kubaki Kijana
Ina antioxidants zinazopambana na free radicals (husababisha kuzeeka). Majani yaliyosagwa yanaweza kutumika kama scrub ya asili.

▪️Kuboresha Macho
Vitamini A husaidia kulinda uwezo wa kuona.

▪️Kuboresha Usingizi
Hutuliza akili na kusaidia kupata usingizi kirahisi.

▪️Kupambana na Mzio (Allergy)
Quercetin husaidia kupunguza dalili za mzio kama kuwashwa ngozi, mzio wa chakula, na pumu.

▪️Kupunguza Cholesterol Mbaya
Husaidia kupunguza LDL na triglycerides.

▪️Kikohozi na Mafua
Kwa sababu ya vitamini C na madini ya chuma, husaidia kutoa makohozi na kupunguza kikohozi (hasa ikichanganywa na asali).

▪️Kuwashwa Mwili
Majani yaliyopondwa hupakwa kwenye eneo husika.

▪️Kung’atwa na Wadudu
Paka majani yaliyosagwa ili kupunguza maumivu.

▪️Afya ya Nywele
Husaidia kupunguza kupotea kwa nywele na kuchochea ukuaji. Spray au oshea nywele zako utaona zinavofumka

▪️Homa ya Taifodi na Malaria
Hutumika jadi kusaidia kupona.

▪️Kupunguza Uzito
Husaidia kupunguza utengenezaji wa mafuta mwilini na kuongeza metabolism.

▪️Matatizo ya Tumbo na Kufunga choo
Ina uwezo wa kupambana na bakteria tumboni.

▪️Vidonda vya Tumbo
Husaidia kulinda ukuta wa tumbo na kupona kwa vidonda.

▪️Kuharisha na Kuhara damu (Dysentery)
Husaidia kutokana na uwezo wake wa kuua vijidudu.

▪️Afya ya Ini (Liver)
Hulinda ini dhidi ya sumu.

▪️Kansa
Ina antioxidants zinazoweza kusaidia kupunguza hatari ya baadhi ya kansa.

▪️Metabolism
Husaidia kurekebisha uchakataji wa virutubisho mwilini.

▪️Afya ya Moyo
Husaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo na kiharusi.

▪️Nguvu za Kiume
Inaweza kusaidia kuongeza uzalishaji wa mbegu za kiume. Tafuna majani yake machanga 

Nguvu za Tendo la Ndoa (Libido)
Inaweza kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume na wanawake.

▪️Chunusi
Husaidia kupunguza chunusi na uvimbe wa ngozi.

▪️Vidonda Vidogo
Husaidia kuzuia maambukizi ukipaka juisi yake.

▪️Maambukizi ya Sikio
Tumia chai iliyopoa.

▪️Homa ya Dengue
Inaaminika kusaidia kuongeza platelet.

▪️Kipindupindu (Cholera)
Ina uwezo wa kupambana na bakteria husika.

▪️Kisukari
Inaweza kusaidia kudhibiti sukari ya damu.

▪️Maumivu ya Jino
Tafuna majani au paka yaliyosagwa.

▪️Fizi Kuvimba na Vidonda vya Mdomo
Tafuna au suuza kwa chai ya majani.

▪️Blackheads
Tumia kama kisafisha ngozi cha asili.

✅️Jinsi ya Kutumia (Dozi):
—Chemsha majani mabichi 7–10 (au makavu 5–6) katika lita 1 ya maji.
AU
—Chemsha kijiko 1 cha unga wa majani katika lita 1 ya maji.

Watu wazima: glasi 1 mara 3 kwa siku
Watoto (kuanzia miezi 6): dozi ndogo kulingana na umri

Wajawazito na Wanaonyonyesha
Watumie kwa kiasi kidogo (nusu ya dozi ya kawaida), na ni muhimu kushauriana na daktari kabla ya kutumia.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Wasifu wa Kizza Besigye

KWA KHERI MAKARANGA UMEUTIMIZA MWENDO...

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

KATI YA WATOTO 7 WA HAYATI MAGUFULI ANAYEJULIKANA ZAIDI NI JESCA

KIKOSI KILICHOITWA TAIFA STARS HIKI HAPA

UBORA UNAONEKANA: BENKI YA NMB YANG'ARA TUZO ZA EUROMONEY 2026

KIJANA WA KINYAKYUSA WA ENZI HIZO, NUSURA AMCHAPE WAZIRI MUONGO BUNGENI

WANAJESHI WAGOMA KWENDA IRAN KUPIGA