SIMUOGOPI TRUMP - PAPA LEO

 Papa Leo XIV amesema ataendelea kupaza sauti dhidi ya vita vinavyoendelea kati ya Marekani na Iran, akisisitiza kuwa migogoro hiyo “haikubaliki” na akimtaka Rais Donald Trump kutafuta njia mbadala ya kuleta amani. 

Amesema jukumu lake kama kiongozi wa kidini si la kisiasa bali ni kuhubiri amani duniani, na kwamba haogopi serikali ya Trump wala shinikizo lolote la kisiasa.

Kwa upande wake, Trump alikosoa uongozi wa Papa Leo akimuita “dhaifu katika sera za kigeni na uhalifu,” na baadaye akasema hadharani kwamba yeye si shabiki wake. 

Pia alidai kuwa kuchaguliwa kwa Papa huyo kulihusiana na uraia wake wa Marekani, akisema kuwa “kama asingekuwa Ikulu ya White House, Leo hangekuwa Vatican.” 

Papa Leo ambaye yuko katika ziara ya siku 11 bara Afrika, amesema kuwa yeye si mwanasiasa ila ni mjumbe wa kueneza amani duniani.

“Siogopi utawala wa Trump, au siogopi kueneza injili ambalo ndilo wajibu wangu na jukumu la kanisa.” Aliwaambia wanahabari .

“Sitaki kujibizana na Trump, kuna watu wengi wanakufa duniani bila hatia, na nadhani ni wakati wa mtu kujitokeza na kupaza sauti na kusema kuna njia bora ya kutatua hili.” Aliongezea Papa Leo. 



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Wasifu wa Kizza Besigye

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

KATI YA WATOTO 7 WA HAYATI MAGUFULI ANAYEJULIKANA ZAIDI NI JESCA

AINA 10 ZA WANAWAKE AMBAO BIBLIA INAKUONYA UWAEPUKE

KIKOSI KILICHOITWA TAIFA STARS HIKI HAPA

UBORA UNAONEKANA: BENKI YA NMB YANG'ARA TUZO ZA EUROMONEY 2026

MAJANI YA MAPERA NA MATUMIZI YAKE YA KITIBA

MCHIMBAJI MDOGO WA DHAHABU AFANYA MAKUBWA KWENYE HUDUMA ZA AFYA