WALIOTAJWA RIPOTI YA CAG KUHOJIWA NA BUNGE

Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu, amefafanua utaratibu utakaotumika katika kuifanyia kazi ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mara baada ya kuwasilishwa bungeni.

Spika Zungu ametoa ufafanuzi huo bungeni leo Aprili 10, 2026, kufuatia Serikali kupitia Wizara ya Fedha Tanzania kuwasilisha mezani ripoti hiyo ya ukaguzi wa hesabu za serikali.

Amesema baada ya ripoti hiyo kuwekwa mezani, Kamati za Kudumu za Bunge zinazoshughulikia usimamizi wa matumizi ya fedha za umma zitaanza kuifanyia kazi kwa kuwahoji maafisa masuuli wa taasisi mbalimbali za serikali ili kutoa ufafanuzi kuhusu hoja zilizobainishwa katika ukaguzi huo.

Spika Zungu amesisitiza kuwa jukumu la Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ni kubaini dosari na mapungufu katika matumizi ya fedha za umma, huku Bunge likiwa na wajibu wa kubaini hatua za moja kwa moja za uwajibikaji na kutoa maazimio yatakayotekelezwa na serikali.

Aidha, amesema Bunge litaendelea kuhakikisha ripoti hiyo inafanyiwa kazi kikamilifu ili kulinda nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na kuimarisha uwajibikaji serikalini.

Awali akiwasilisha taarifa hiyo bungeni, Naibu Waziri wa Fedha, Laurent Luswetula, amesema ripoti hiyo inahusisha ukaguzi wa fedha za miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2025, ukaguzi wa hesabu za mashirika ya umma pamoja na ukaguzi wa ufanisi wa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi wasiojiweza.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Wasifu wa Kizza Besigye

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

KATI YA WATOTO 7 WA HAYATI MAGUFULI ANAYEJULIKANA ZAIDI NI JESCA

KIKOSI KILICHOITWA TAIFA STARS HIKI HAPA

AINA 10 ZA WANAWAKE AMBAO BIBLIA INAKUONYA UWAEPUKE

UBORA UNAONEKANA: BENKI YA NMB YANG'ARA TUZO ZA EUROMONEY 2026

MAJANI YA MAPERA NA MATUMIZI YAKE YA KITIBA

WANAJESHI WAGOMA KWENDA IRAN KUPIGA

MCHIMBAJI MDOGO WA DHAHABU AFANYA MAKUBWA KWENYE HUDUMA ZA AFYA