Mbunge wa Viti Maalumu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Dodoma, Dkt. Neema Majule ameishauri Serikali kuwashirikisha wanawake katika kupanga mipango, kusimamia na kufanya Tathmini ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Pia ameomba uundwe mfuko maalumu utakaosimama kama dhamana ya kuwapatia mikopo wanawake kwa ajili ya mitaji ya kuanzisha miradi mbalimbali itakayo wakwamua kiuchumi.
Pamoja na mambo mengine, Dkt.Majule ameyasema hayo alipokuwa akichangia mjadala wa makadirio ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, bungeni Dodoma Aprili 10, 2026.
Dkt. Majule akipongezwa na wabunge wenzie.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203
Comments