MWANYIKA ATETA NA MKURUGENZI MKUU WA NHC BUNGENI

Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika (kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Hamad Abdallah kwenye viunga vya Bunge Mei 28, 2026. 
                                       .............
Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo ikiambatana na Menejimenti ya Shirika hilo iliwahi tembelea mkoa wa Njombe kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya makazi na biashara.

Ziara hiyo ilifanyika kwa ushirikiano na Kamishna wa Ardhi wa Mkoa wa Njombe pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Bw. Christopher Aloyce Sanga.

Kupitia ziara hiyo, Bodi ilipata nafasi ya kuona maeneo ambayo Halmashauri ya Wilaya ya Njombe inapendekeza kushirikiana na NHC katika kuendeleza miradi ya kimkakati ya majengo ya biashara na nyumba bora za kisasa.

Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Hamad Abdallah, alisema NHC inatambua Njombe kama mkoa wenye fursa kubwa za uwekezaji, hasa katika sekta ya makazi, na Shirika lipo tayari kushirikiana na Halmashauri ili kuhakikisha miradi hiyo inaleta manufaa kwa wananchi na kuongeza mapato ya ndani.



 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

Wasifu wa Kizza Besigye

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA