Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo ameitahadharisha Wizara ya Maji kuwa makini kutumia maji ya maziwa hayo kuwa chanzo pekee yatakayotumika kwenye Gridi ya Taifa ya Maji kwani hata historia maziwa hayo yamewahi kauka kwa mujibu wa utafiti wa kijiolojia, Ziwa Tganzaganyika haliwahi kauka.
Ametoa tahadhari hiyo alipokuwa akichangia hoja wakati wa semina kwa wabunge kuhusu Mpango ulivyo wa utekelezaji wa Gridi Taifa ya Maji.
Semina hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Maji na kuongozwa na Spika wa Bunge , Mussa Azzan Zungu ilifanyika kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa bungeni Dodoma Aprili 30, 2026.
Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu akiongoza kikao hicho.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akijibu hoja za wabunge. Kulia ni Spika wa Bunge, Mussa Zungu.
Spika mstaafu ambaye ni Mbunge wa Uyole, Dkt. Tulia Ackson akiwa na Mbunge wa Busokelo, Lutengano Mwalwiba wakisikiliza kwa makini hoja mbalimbali.
Wabunge wakiwa katika semina hiyo.
Eng. Aron JosephMkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph akiwa na baadhi ya watumishi wa mamlaka hiyo.IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203








Comments