MWALUNENGE ATAKA MIRADI YA BARABARA MBEYA IKAMILIKE KWA WAKATI

 Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Patrick Mwalunenge amesema ujenzi wa barabara mkoani Mbeya una umuhimu mkubwa kwa uchumi wa taifa kutokana na mkoa huo kuwa njia kuu ya usafirishaji wa mizigo kwenda nchi jirani.


Akichangia bungeni, Mwalunenge alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya barabara ikiwemo barabara ya njia nne jijini Mbeya na fidia kwa wananchi wa mradi wa barabara ya mzunguko.


Ameiomba Wizara ya Ujenzi kuhakikisha wakandarasi wanaendelea na kazi ili miradi ikamilike kwa wakati, huku akisisitiza umuhimu wa barabara ya Makongorosi–Lwango kwa biashara na uchumi.


Aidha, ameikosoa Sheria ya Manunuzi ya Umma akidai inachelewesha miradi na kuwanyima nafasi wakandarasi wazawa. Ameshauri serikali kuweka mazingira ya kuwajengea uwezo wazawa na wahandisi wa Kitanzania ili fedha za miradi ziendelee kukuza uchumi wa ndani.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

TANZIA;.KWA KHERI DADA YETU MPENDWA EDITHA, TASNIA IMEPATA PIGO

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

RAIS SAMIA AWASILI IRINGA KWENDA MEI MOSI NJOMBE