JKT YAREJEA WITO KWA VIJANA WALIOCHELEWA KURIPOTI MAKAMBINI, WARUHUSIWA KURIPOTI HADI JUNI 15, 2026

Na Mwandishi wetu Michuzi TV

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetoa nafasi ya mwisho kwa vijana waliohitimu elimu ya sekondari ngazi ya Kidato cha Sita mwaka 2026 na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria, lakini bado hawajaripoti katika makambi waliyopangiwa.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 12, 2026, jijini Dodoma na Makao Makuu ya JKT, vijana hao wametakiwa kuripoti kuanzia leo hadi Juni 15, 2026 ili kuendelea na mafunzo yao.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo JKT, Peter Mnyani, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Rajabu Nduku Mabele.

JKT imeeleza kuwa vijana ambao hawakufanikiwa kufika katika makambi waliyoelekezwa awali wanapaswa kuripoti katika kambi za JKT zilizo karibu na maeneo wanayoishi ili kurahisisha usajili na kuendelea na mafunzo.

Hata hivyo, Jeshi hilo limefafanua kuwa utaratibu huo hauhusishi vijana wanaotakiwa kuripoti katika Kambi ya Makutupora JKT Camp, Kambi ya Ruvu JKT Camp pamoja na Kambi ya Chuo cha Uongozi Kimbiji, ambazo hazijajumuishwa katika mwongozo huo wa kuripoti kwenye kambi zilizo karibu.

JKT imewasisitiza vijana wote husika kutumia fursa hiyo ya nyongeza ya muda kuhakikisha wanaripoti ndani ya kipindi kilichotolewa ili kutimiza wajibu wao wa kujiunga na mafunzo kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Wasifu wa Kizza Besigye

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda