MAPENDEKEZO 121 KATI YA 727 YA KODI, TOZO, ADA YAKUBALIWA BAJETI KUU

 Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar akielezea mbele ya vyombo vya habari kuhusu maboresho ya kodi, ada na tozo mbalimbali, ambapo hadi wanafunga dirisha la kupokea maoni kwa mwaka 2026, jumla ya mapendekezo 727, ya kikodi, kisheria, na hata ya kiutawala yalipokelewa.

Pamoja na mambo mengine, ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandhishi wa habari jijini Dodoma Juni 10, 2026, kuelezea kwa ufupi kuhusu mapendendekezo ya muelekeo wa Bajeti Kuu ya Serikali itakayowasilishwa rasmi bungeni kesho Alhamisi juni 11, 2026.. Amesema kuwa uchakataji wa mapendekezo hayo ulianza mwezi Februari 2026 kupitia Kamati ya Wataalam ya Maboresho ya Kodi (Taskforce on Tax Reforms) inayojumuisha wawakilishi kutoka Serikali Kuu, Taasisi zake na Sekta Binafsi. "Kati ya mapendekezo hayo, jumla ya mapendekezo 125 yalikubaliwa kama yalivyowasilishwa; 121 yalikubaliwa baada ya kuboreshwa; 295 yalikataliwa; mapendekezo 107 ilielekezwa na kamati ya maboresho ya mfumo wa kodi (Task Force on Task Reforms) kuwasilishwa kwa Wizara/Taasisi husika kwa ajili ya kutolewa ufafanuzi au kufanyiwa uchambuzi; na yale ambayo hayajafanyiwa maamuzi kutokana na ukosefu wa takwimu au taarifa za kutosha ni 47. '"amefafanua Waziri.

Aidha, mapendekezo ya maboresho ambayo yapo katika hatua mbalimbali za utekelezaji Serikalini ni 32.

Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar.

Baadhi ya maafisa watendaji wa wizara hiyo.

Waandishi wa habari wakiwa kazini.



IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA- 0754264206

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA

Wasifu wa Kizza Besigye

NGUVU YA UJASUSI WA TANZANIA KITOVU CHAKE NI IRINGA TANGU ENZI ZA MKWAWA