AFRIKA NA WAAFRIKA NI LAZIMA TUAMKE. TUMELALA MNO!



 Afrika na Waafrika ni lazima tuamke. Tumelala mno! Tuliuzwa sokoni kama bidhaa wakati wa utumwa;


Tulinyonywa, kukandamizwa na kuvuliwa utu wetu, wakati wa ukoloni;


Tumeendelea kuhadaiwa na mfumo wa ukoloni mamboleo, kwamba sisi ni maskini tunaohitaji kusaidiwa;


Unasaidiwaje na walewale waliokuuza sokoni kama kuku, wakati walikuja kuiba rasilmali zako, ambazo wanazihitaji na kuzifuata hadi leo?


Tafiti zinathibitisha kuwa kila Shilingi moja inayokuja Afrika kama msaada, wao  wanachukua Shilingi mbili!Hapa ni nani anamsaidia mwingine?


Imekuwaje leo, wasomi wa Afrika hawazungumzii kwa sauti suala hili, wakati liko wazi? Je, ni kwa sababu wanalamba asali ya mabeberu?


Inakuwaje John Perkins, ktk vitabu vyake vya 'Confessions of an Economic Hitman' anaeleza wazi michezo wanayoicheza mabeberu Afrika na bado Waafrika hawaelewi na hawaamki?


Je, ni kwamba Waafrika ni watu wasioweza kung'amua mambo au ni kwamba wamepigwa juju na mabeberu?


Je, ni kwa nini ktk historia niliyosoma kuhusu Waafrika, ninakutana na visa vingi vya usaliti?


Viongozi wote wa Afrika waliopambana na ukoloni na ubeberu, walisalitiwa na Waafrika wenzao; ni kwa nini? Kila kiongozi mzalendo wa Afrika alisalitiwa na Mwafrika mwenzake; ni kwa nini?


Ni kwa nini ni Waafrika tu waliosaliti utamaduni wao kwa kuendelea na imani za kigeni, majina ya kigeni, lugha za kigeni, fikra za kigeni, elimu ya kigeni, n.k. kwani Waafrika siyo binadamu kamili?


Ni kwa nini Waafrika ambao Bara lao lina rasilmali nyingi, wanaongoza kwa migogoro, machafuko na vita na wakati wanufaika wakiwa ni mabeberu?


Ni kwanini Afrika inapopata viongozi wazalendo kama (miaka ya karibuni) JPM na SSH wa Tanzania - waliojipambanua ktk kuinua maisha ya wananchi wao kwa kutumia rasilmali za Nchi - ni lazima wakumbane na dhahama ya kusalitiwa, kubagazwa na kutakiwa kuondolewa?


Je, endapo kwa miongo zaidi ya 6 ya uhuru wa nchi za Afrika, demokrasia ya kubadilishana vyama madarakani ilipaswa kuwa suluhisho la matatizo na changamoto za Afrika, ni kwa nini Tanzania (ambayo haijabadili vyama madarakani) inafanya vizuri zaidi kiuchumi na kimaendeleo, kuliko nchi zilizobadilisha vyama madarakani Afrika?


Najaribu kuendelea kusisitiza umuhimu wa Waafrika kuendelea kujiuliza; changamoto muhimu za Afrika ni zipi!


Sasa hivi Tanzania mnaendelea kusikiliza watu wanaowachochea kuchukiana, kukasirikiana na kusambaratishana! 


Je, wanawaeleza namna bora ya kujenga Taifa lililosambaratishwa kutokana na chuki za mihemuko ya wakati?


Wanaelewa sawasawa yaliyotokea Rwanda mwaka 1994 na athari zake kwa umoja wa kitaifa?


Je, waliowahimiza kuvunja Taifa Oktoba 29, waliwaelekeza vijana namna ya kuishi kati ya tarehe hiyo na tarehe 4 Novemba? 


Kabla ya kuendelea kuwahimiza vijana kuvunja amani tena, waliwauliza waliishije kuanzia tarehe 29 Oktoba hadi tarehe 4 Novemba?


Je, Watanzania waliishi maisha ya aina gani kati ya tarehe 29 Oktoba na 4 Novemba? Je maisha yale yaliwakilisha utamaduni wa Watanzania?


Wanaohamasisha sasa maandamano ya Sabasaba, wametafakari yaliyotokea Oktoba 29 na athari zake kwa maisha ya Watanzania? 


Je, wametafakari kwa kina kubaini Watanzania wana hisia gani kuhusu dhahama iliyowakuta baada ya Oktoba 29? 


Je, wamejiuliza ni kwa nini wito wa maandamano ya tarehe 9 Disemba na tarehe 25 Disemba ulipuuzwa na Watanzania?


Bado sijaelewa ni kwa nini uongozi wa CHADEMA hauoneshi nia ya kupokea mkono wa maridhiano unaohubiriwa na Serikali na Chama Tawala! Dhamira yao ni nini?


Ninaamini - pamoja na changamoto za demokrasia yetu - tunapaswa kutafakari, kujadili na kukubaliana namna bora ya kuishi pamoja, kwa misingi ya Kitanzania.


Tunapaswa kujua kwamba - kama alivyobainisha Charles Darwin - viumbe vyote duniani vinatafuta namna ya kujinusurisha kwa sababu rasilmali ni chache!


Inasikitisha kwamba - hadi sasa - ni Waafrika pekee wanaoonesha jitihada kubwa za kusaidia viumbe vingine kujinusurisha, wakati wao wakikubali kusambaratishwa!


Ninaamini suala la kuachiwa kwa ndugu yetu Tundu Lisu, linazungumzika, kama ilivyokuwa kwenye kuachiwa kwa Mwenyekiti, Freeman Mbowe.


Lakini makundi yote ktk Taifa letu yanapaswa kuonesha dhamira ya uungwana wa kuzungumza na kusikilizana! Inawezekana!

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Wasifu wa Kizza Besigye

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda