WAZIRI MKUU APONGEZA NMB KWA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIFEDHA VIJIJINI

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ameipongeza Benki ya NMB kwa kuendelea kusogeza huduma za kifedha karibu na wananchi kupitia matumizi ya teknolojia na mkakati wa Rural Banking, akisema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara na kupunguza gharama za miamala ya kifedha.

Akimkaribisha Waziri Mkuu katika banda la NMB kwenye Maonesho ya Nanenane, Mkuu wa Idara ya Biashara za Serikali wa benki hiyo, Bi. Vicky Bishubo, alisema NMB imeendelea kuwekeza katika sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji, ikiwa tayari imetoa mikopo yenye thamani ya Sh. trilioni 2.3 kwa sekta hizo.

Alisema benki hiyo pia imewawezesha vijana kupata mikopo ya hadi Sh. milioni mbili kupitia teknolojia bila dhamana wala kwenda tawi, huku huduma za Rural Banking zikiendelea kufika katika masoko na minada ya biashara na mifugo katika maeneo mbalimbali nchini.

Mbali na huduma za kifedha, NMB inaendelea kutoa elimu ya fedha kupitia NMB Kijiji Day na kushirikiana na vyuo vikuu kuwajengea vijana ujuzi unaohitajika katika uchumi unaotegemea teknolojia na ubunifu.



 Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Biashara za Serikali wa Benki ya NMB, Bi. Vicky Bishubo, alipotembelea banda la benki hiyo katika Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nanenane yanayoendelea kwenye Viwanja vya John S. Malecela, Nzuguni mkoani Dodoma jana. NMB ni mdhamini wa maonesho hayo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KATIKA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA.

YANGA YAMPOTEZA MAMA FATMA KARUME MWANA YANGA KINDAKI NDAKI

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA

DKT. TULIA ATAJA MAFANIKIO YAKE AKIWA RAIS WA IPU