Dkt. Tulia awatakia Heri Wajumbe uchaguzi wa Rais Mpya IPU.

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge Mstaafu, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amewatakia heri Wajumbe wa Mkutano wa 153 wa umoja huo wanapojiandaa kumchagua Rais mpya wa umoja huo.

Mheshimiwa Dkt. Tulia alikuwa akizungumza katika hafla ya usiku wa utamaduni ambayo Bunge la Tanzania limeaandaa kwa ajili ya washiriki wa Mkutano wa IPU.

Uchaguzi wa Rais mpya wa IPU utafanyika kesho Oktoba 9, 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) ambako Mkutano huo unafanyika.

"Najua kesho tutaandika historia nyingine ya kumchagua Rais mpya wa  IPU, nimatumaini yangu mtampata Rais bora na hivyo kuendelea kufurahia mtangamano wetu," amesema.

Akizungumzia Mkutano wa 153 unaoendelea jijini Arusha amesema Tanzania imetengeneza rekodi ya dunia kwa mkutano huo kuongozwa na watanzania wawili ambaye ni yeye Rais wa IPU pamoja na Rais wa Mkutano wa 153 ambaye ni Spika wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu.

Aidha, alimshukuru Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha Mkutano wa 153 kufanyika Tanzania, Spika wa Bunge Mheshimiwa Zungu na Katibu wa Bunge Ndugu Baraka Leonard kwa maandalizi mazuri.

 "Asanteni wote kwa ukarimu ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuhakikisha wageni wetu wanakuwa salama hadi kufkia muda huu," amesema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa IPU, Anda Filip amemshukuru Rais wa IPU Dkt. Tulia, Spika Mhe. Zungu kwa ukarimu na mapokezi mazuri wote wa mkutano.


P





 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KATIKA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA.

YANGA YAMPOTEZA MAMA FATMA KARUME MWANA YANGA KINDAKI NDAKI

𝐌𝐉𝐔𝐄 𝐊𝐀𝐂𝐇𝐄𝐑𝐎 𝐌𝐙𝐄𝐍𝐀

MVUA ZA EL NINO ZINASABABISHWA NA NINI?.