GEWOMA: LESENI TATU ZA MADINI KUWAFUNGULIA WACHIMBAJI FURSA GEITA


NA MWANDISHI WETU, GEITA


WACHIMBAJI wadogo wa madini ya dhahabu mkoani Geita wamekabidhiwa leseni tatu za uchimbaji zinazohusisha eneo lenye ukubwa wa takribani ekari 60, hatua inayotarajiwa kuwawezesha kuanza shughuli za uchimbaji rasmi na kuongeza fursa za kiuchumi.


Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo leo Oktoba 2,2026 kwenye Maonesho ya Tisa ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea Katika Viwanja vya Dkt.Samia Suluhu Hassan mkoani Geita.

 Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Geita (GEWOMA), Asia Masimba, amesema kukabidhiwa kwa leseni hizo ni hatua muhimu kwa wachimbaji wadogo, ambao wamekuwa wakihitaji fursa za kupata maeneo ya uchimbaji na kuendesha shughuli zao kwa utaratibu unaotambulika kisheria.


Akizungumza baada ya kukabidhiwa kwa leseni hizo, Masimba ameeleza furaha ya wachimbaji hao, akisema hatua hiyo imeongeza matumaini ya kuanza kazi katika maeneo waliyopewa na kutumia fursa zilizopo katika sekta ya madini.


Amesema wachimbaji hao wameishukuru Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Geita na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa hatua ya kuwawezesha kupata leseni hizo.


Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa wakati wa tukio hilo, leseni hizo tatu zinahusisha eneo la takribani ekari 60, huku wachimbaji wakieleza utayari wa kuanza maandalizi ya shughuli za uchimbaji mara baada ya kukamilika kwa maonesho.


Hatua hiyo inatarajiwa kufungua fursa kwa wachimbaji hao kushiriki zaidi katika shughuli za uzalishaji wa dhahabu na kukuza shughuli zao za kiuchumi.


Hata hivyo, mafanikio ya fursa hiyo yatategemea maandalizi ya uchimbaji, upatikanaji wa mitaji, matumizi ya teknolojia sahihi na uzingatiaji wa sheria na kanuni za usalama migodini.


Wachimbaji hao wameeleza matumaini yao kuwa leseni hizo zitakuwa mwanzo wa safari mpya ya maendeleo, huku wakitoa shukrani kwa viongozi na wadau waliohusika katika kufanikisha upatikanaji wake.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

𝐌𝐉𝐔𝐄 𝐊𝐀𝐂𝐇𝐄𝐑𝐎 𝐌𝐙𝐄𝐍𝐀

KATIKA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA.

YANGA YAMPOTEZA MAMA FATMA KARUME MWANA YANGA KINDAKI NDAKI

MVUA ZA EL NINO ZINASABABISHWA NA NINI?.

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU