RAIS WA FAJ, VIONGOZI WA JOWUTA WAKUTANA


Rais wa Shirikisho la Waandishi wa Habari Afrika (FAJ), katikati akiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (JOWUTA), Selemani Msuya kulia na Naibu Katibu Mkuu Said Mmanga kushoto


NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Shirikisho la Vyama vya Waandishi wa Habari Afrika (FAJ), Omar Farouk Osman, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Chama cha Wafanyakazi kwenye vyombo vya Habari nchiji (JOWUTA) ambapo katika mazungumzo yao amekitaka chama hicho kuongeza kasi ya kusajili wanachama ili kujenga nguvu ya ya ushawishi nje ya mipaka ya Tanzania.


Omar ametoa kauli hiyo Oktoba 6, 2026 katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam alipokutana na Katibu Mkuu wa JOWUTA Selemani Msuya na Naibu Katibu Mkuu Said Mmanga.


Amesema JOWUTA ni moja ya chama cha wanahabari kinachokuwa kwa kasi, hivyo kinapaswa kuongeze juhudi ya kusajili wanachama kwa kuwa ndiyo nguvu ya chama cha wafanyakazi.


Amesema FAJ inaitazama Tanzania kama nchi ya mkakati kutokana na ushawishi wake katika masuala mbalimbali barani Afrika, hivyo JOWUTA haina budi kuwa na nguvu imara inayotokana na idadi ya wanachama wake.


Sanjari na hilo alisisitiza umuhimu wa chama hicho kulipa ada na michango yake katika Shirikisho la Vyama vya Waandishi wa Habari la Kimataifa (IFJ) kwa wakati ili iendelee kufaidika na fursa mbalimbali zinazotolewa na shirikisho hilo.


"Nashukuru sana kwa kuonana na nanyi hapa, Mwenyekiti ameniambia yupo Nairobi kikazi, endeleeni kusajili wanachama wapya na kulipa ada kwa wakati ili muwe hai ndani ya IFJ na kupata nafasi ya kushiriki mikutano, mafunzo na miradi ya maendeleo inayoendeshwa na FAJ," amesema.


Omar ameipongeza JOWUTA kwa kuanzisha program ya kuhamamisha waandishi wa habari walio katika mfumo rasmi na wale walio nje ya mfumo huo kujiunga na utaratibu wa Hifadhi ya Jamii kwa Hiyari ambayo inatekelezwa kwa ushirikiano na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).


Pia amekita chama hicho kuendelea kutoa mafunzo kwa wanachama wake kila wanapopata fedha, hali ambayo itavutia waandishi kujiunga kwa wingi.


Kwa upande wake Katibu Mkuu wa JOWUTA Selemani Msuya amemshukuru Rais Omar kutenga muda wake na kuzungumza nao, huku akisisitiza kuendelea na usajili wanachama na NSSF na mifuko mingine ambayo itaifanya kesho ya mwandishi kuwa salama.


Msuya ameahidi kushirikiana na viongozi wenzake katika kuhakikisha wanaongeza wanachama na kulipa ada kama taratibu zinavyoelekeza.


Pia ameiomba FAJ kutenge bajeti kwa ajili ya mafunzo kwa waandishi wa habari wa Tanzania.




Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

𝐌𝐉𝐔𝐄 𝐊𝐀𝐂𝐇𝐄𝐑𝐎 𝐌𝐙𝐄𝐍𝐀

KATIKA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA.

YANGA YAMPOTEZA MAMA FATMA KARUME MWANA YANGA KINDAKI NDAKI

MVUA ZA EL NINO ZINASABABISHWA NA NINI?.