Askofu Mkuu wa Kanisa la Karmel Assembilies of God Tanzania (KAG), Dkt. Evance Chande ametoa machozi alipokuwa akielezea mambo magumu yenye mateso ndani ya miaka 6 katika utumishi wake wa miaka 40 ya kuhubiri Injili.
Tukio hilo limetokea katika ibada maalumu ya kumshukuru Mungu kwa matendo makubwa aliyomfanyia ikiwemo kumnusuru kifo iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa hilo Ipagala jijini Dodoma Novemba 15, 2026.
Ibada hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa dini wa ndani na nje ya Nchi miongoni mwao wakiwemo maaskofu, wachungaji, wainjilisti, viongozi wa serikali na vyama vya siasa pamoja na waumini ambao kwa muda wote alipokuwa anakumbana na changamoto hawkumuacha waliendelea kuwa nawe na kumuombea.
Akofu Chande akielezea changamoto mbalimbali alizopitia katika utumishi wake wa kuhubiri injili.
Askofu Chande akiwa na Baba Mlezi wake. Mwinjilisti Mstaafu George Banali. (kushoto) na Makamu Askofu Mkuu wa KAG, Kelvin Mringo.
Baadhi ya waumini na wageni waalikwa.






Comments