BAADA YA KUPOKEA CHETI KUPATA CHETI CHA PONGEZI KUTOKA KWA PAPA, SASA NIPO TAYARI KUONDOKA DUNIANI- EDA SANGA NIPO TAYARI
Miaka 50 ya ndoa haikuwa rahisi. Kulikuwa na nyakati za kulia na kucheka, changamoto na mafanikio. Lakini kwa kujitolea na kushikamana, yote tuliyapitia pamoja na kuyashinda," anasema Mama Edda Sanga kwa sauti iliyojaa bashasha.
Akiwa na umri wa miaka 79, Edda Sanga aliyetoa mchango mkubwa katika historia ya uandishi wa habari Tanzania anajivunia kupokea cheti cha pongezi 2024 kutoka Vatican kwa aliyekuwa kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis.
'Kuna zawadi kubwa kuliko hiyo? Namimi nilisema ingekuwa kuna namna ya kumuomba Mungu kwamba baada ya kupata hiki cheti sasa baba niko tayari kuondoka katika dunia hii,nimemaliza kazi yangu'
'Maisha ya watu wawili hayawezi kuwa a bed of roses' alisisitiza Edda Sanga kuwa maisha ya ndoa sio raha mustarehe tu.

Comments