Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mhe. Mary Pius Chatanda (MCC), tarehe 16 Novemba 2026, amezungumza na kuwaponga wanawake wajasiriamali wanufaika wa mikopo ya uwezeshaji katika eneo la Paje, Mkoa wa Kusini Unguja, wakati wa ziara ya Kamati ya Utekelezaji ya UWT Taifa.
Akizungumza na wajasiriamali na kina mama wa Paje ,Chatanda amewapongeza kwa kutumia fursa ya mikopo kuendeleza shughuli zao za kiuchumi na kuwataka waendelee kuchangamkia fursa mbalimbali za maendeleo zinazotolewa na Serikali ili kukuza mitaji yao, kuongeza kipato na kuboresha maisha yao.
Comments