JESHI LA MAGEREZA NA VETA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA URASIMISHAJI UJUZI KWA WAFUNGWA


NA SSGT MAWAZO MTONDO - DODOMA

MKUU wa Sehemu ya Viwanda wa Jeshi la Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) Dkt. Uswege Mwakahesya, leo Novemba 18, 2026, ameongoza kikao cha maandalizi ya hafla ya kuwatunuku vyeti wafungwa 481 waliohitimu mafunzo ya ufundi kupitia Mfumo Usio Rasmi wa Mafunzo (RPL) chini ya Programu ya Mama Samia.


Hafla hiyo inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa Novemba 2026 katika Viwanja vya Gereza Karanga, mkoani Kilimanjaro, na itahusisha pia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano kati ya Jeshi la Magereza na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).


Ushirikiano huo unalenga kutambua, kuthibitisha na kurasimisha ujuzi wa wafungwa ili kuwawezesha kutumia ujuzi huo kujiajiri au kuajiriwa wanaporejea katika jamii.






Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UJUE UKWELI KUHUSU JIJI LA MBEYA (GREEN CITY)

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA

KAMISHNA DKT.BADRU ATUA KAMBI YA TIMU YA NGORONGORO KAMA SELEMANI MWALIMU

TIMU YA NGORONGORO KAMA DOUMBIA