NDEJEMBI AAGIZA FIDIA KULIPWA, ATOA SIKU 60 KUKAMILISHA MRADI WA MAJI MADANGWA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, Novemba 14, 2026, ameanza ziara ya kikazi mkoani Lindi kwa kuzungumza na wananchi wa Madangwa, Jimbo la Mtama, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika mikoa ya Kusini.



Madangwa ni kituo cha kwanza cha ziara yake mkoani Lindi baada ya kutoka mkoani Mtwara. Akiwasili katika eneo hilo, alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Adam Malima, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, wabunge wa Mkoa wa Lindi pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM na Serikali.


Akiwa Madangwa, Makamu wa Rais ameiagiza Wizara ya Ujenzi kuanza kulipa fidia kwa wananchi waliopisha maeneo yao kwa ajili ya ujenzi wa barabara, ikiwezekana malipo hayo yafanyike kwa awamu.


Aidha, Wizara ya Maji imeahidi kutoa Sh milioni 500 kwa ajili ya ukarabati wa mradi wa maji ili huduma hiyo irejeshwe na kupatikana kwa wananchi ndani ya miezi miwili.


Katika hatua nyingine, Wizara ya Kilimo imeahidi kuhakikisha salfa ya unga kwa ajili ya zao la korosho inawafikia wakulima kabla ya Machi 2027.


Makamu wa Rais alianza ziara ya siku saba katika mikoa ya Kusini Novemba 9, 2026, akitembelea mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza pamoja na kutatua kero za wananchi.









Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UJUE UKWELI KUHUSU JIJI LA MBEYA (GREEN CITY)

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA

KAMISHNA DKT.BADRU ATUA KAMBI YA TIMU YA NGORONGORO KAMA SELEMANI MWALIMU

TIMU YA NGORONGORO KAMA DOUMBIA