NDEJEMBI AMWAKILISHA RAIS SAMIA UFUNGUZI WA TMIC 2026

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, anamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania (TMIC 2026), unaofanyika kuanzia Novemba 19 hadi 21, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo umewakutanisha zaidi ya wadau 1,700 kutoka ndani na nje ya nchi kujadili fursa za uwekezaji, kuongeza uchakataji wa madini nchini, kukuza viwanda, ajira na mapato ya Taifa.

Majadiliano yanajikita katika fursa za uwekezaji kwenye madini ya dhahabu, kinywe, nikeli, shaba, madini adimu na niobiamu, pamoja na kuimarisha ushiriki wa wachimbaji wadogo na kampuni za Kitanzania katika mnyororo wa thamani wa sekta ya madini.








Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UJUE UKWELI KUHUSU JIJI LA MBEYA (GREEN CITY)

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA

TIMU YA NGORONGORO KAMA DOUMBIA

KAMISHNA DKT.BADRU ATUA KAMBI YA TIMU YA NGORONGORO KAMA SELEMANI MWALIMU