RAIS SAMIA AFANIKISHA KUJENGA DARAJA LA KISASA MOHORO

  Afisa Tarafa ya Mohoro iliyopo Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani Ndugu Bwanku M Bwanku leo Jumatano Novemba 18, 2026 ametembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mohoro linalokatisha kwenye Mto Mohoro unaomwaga maji yake Bahari ya Hindi. Eneo hili limetesa na kuua wananchi wengi kwa miaka mingi hasa nyakati za mvua ambapo Mto ulijaa na daraja lililopo ni dogo maji yalifunika hivyo kuvuka ilikua lazima utumie mtumbwi au boti.


Kumaliza changamoto hiyo, ndipo Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inajenga daraja la kisasa refu la Mita 275 na hata mvua inyeshe vipi na Mto kujaa wananchi watapita bila changamoto yoyote ile. Hizi ni jitihada za Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye baada ya kilio hiki cha muda mrefu alijenga hoja na kufanikisha ujenzi wa Daraja hili la kisasa.


Afisa Tarafa Ndugu Bwanku ameongozana na Mtendaji wa Kata ya Mohoro Bi. Hilda Kuboja pamoja na Mtaalamu wa vipimo wa mradi huo Ndugu Rajabu Athumani kutembelea kuona maendeleo ya mradi huo uliofika asilimia 75.


Licha ya kurahisisha shughuli za wananchi, kukamilika kwa Daraja hili itakua msaada mkubwa wa kuchochea utalii kwenye eneo la Mbwela kuliko na bichi nzuri za Bahari ya Hindi, kuchochea shughuli za kilimo kwani upande wa pili kunafanyika kilimo cha mpunga, matikiti, korosho, maembe huku likiunganisha Wilaya za Rufiji na Kibiti kuelekea Dar es Salaam na upande wa mkoa wa Lindi.


"Daraja hili ni ndoto ya wana Mohoro na Rufiji iliyosubiri miaka mingi sana, watu wamekufa hapa, shughuli za watu zilisimama sana, sasa Serikali ya Rais Samia imefanikisha. Naomba muendelee kufanya kazi kila siku ili mkimbizane na mvua za El nino zinazotajwa ili kufikia mwanzoni mwakani liishe wananchi waanze kunufaika kiuchumi na kijamii". Alisema Ndugu Bwanku alipotembelea mradi na kuongea na mafundi walioko site wakiendelea na kazi.




Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UJUE UKWELI KUHUSU JIJI LA MBEYA (GREEN CITY)

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA

TIMU YA NGORONGORO KAMA DOUMBIA

KAMISHNA DKT.BADRU ATUA KAMBI YA TIMU YA NGORONGORO KAMA SELEMANI MWALIMU