Kwa vipindi tofauti, watendaji kutoka Tanzania na Uganda wamekuwa wakijadili utekelezaji wa makubaliano yetu. Leo, nikiwa katika ziara nchini Uganda, nimekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wangu, Rais wa Uganda, Mheshimiwa Yoweri Museveni.
Tumefarijika kuona hatua zilizopigwa katika utekelezaji wa makubaliano hayo, hususan katika sekta za biashara, miundombinu, nishati na usafirishaji.
Nimemweleza na kuikaribisha Uganda kuungana na Tanzania katika juhudi za kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji, ikiwemo upanuzi wa bandari, ujenzi wa meli, barabara, reli ya kisasa na usafiri wa anga, ili kurahisisha upatikanaji wa masoko ya kikanda na kimataifa.
Aidha, nimempongeza Rais Museveni kwa hatua ya Uganda kuwa nchi ya kwanza kuanza ujenzi wa Ofisi za Ubalozi wake katika Mji wa Serikali wa Mtumba, jijini Dodoma, hatua inayotarajiwa kuhamasisha mataifa mengine kuwekeza katika eneo hilo.
Comments