WANANCHI WAJITOKEZA HOSPITALI YA TUMBI KUCHUNGUZA AFYA ZAO KUPITIA MADAKTARI BINGWA NA BOBEZI


MWANDISHI WETU, KIBAHA


KAMBI ya matibabu ya madaktari bingwa na bobezi imeanza leo kwa wananchi wengi kujitokeza ili kuchunguzwa afya zao.


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Stanslaus Nyongo akizundua  kambi ya matibabu ya madaktari bingwa na bobezi ya kanda ya Kati amesema kuwa imesogeza huduma za afya kwa wananchi ikiwa ni mpango wa Rais wa kutoa huduma bora na kwa urahisi.


Nyongo ameyasema hayo kwenye Hospitali ya Mkoa wa Pwani Tumbi wakati akizindua kambi ya matibabu bingwa na bobezi kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani kuanzia leo Novemba 16 hadi 20 mwaka huu.


Amesema kuwa kama inavyojulikana huduma za kibingwa na bobezi hupatikana kwenye baadhi ya hospitali na kwa nyakati maalum.


Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Ukio Kusirye alisema kuwa tayari kambi ya madaktari bingwa na bobezi ya mabusha imefanyika Wilayani Kibaha ambapo imetolewa bure.


Kusirye amesema kuwa wanaendelea na utambuzi kwa ajili ya kambi ya macho kwenye Wilaya za Kisarawe na Mafia.


Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi Amani Malima amesema kuwa mwitikio wa watu kujitokeza ni mkubwa ambapo 600 wamejitokeza kwenye siku ya kwanza kati ya siku tano za kambi hiyo.


Malima amesema kuwa baadhi ya huduma zitatolewa bure ikiwa ni pamoja na kumuona daktari kisukari moyo ini mtoto wa jicho miwani na baadhi ya dawa.



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UJUE UKWELI KUHUSU JIJI LA MBEYA (GREEN CITY)

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA

KAMISHNA DKT.BADRU ATUA KAMBI YA TIMU YA NGORONGORO KAMA SELEMANI MWALIMU

TIMU YA NGORONGORO KAMA DOUMBIA