WAZIRI MKUU DKT MWIGULU KUZINDUA KITAMBULISHO CHA TAIFA KILICHO BORESHWA

 



NA MWANDISHI WETU KIBAHA.


WAZIRI Mkuu  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mwigulu Nchemba anatarajiwa kumwakilisha Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwenye uzinduzi wa kitambulisho cha taifa kilichoboreshwa


Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Stanslaus Nyongo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha ambapo uzinduzi huo utafanyika Stendi ya zamani ya Maili Moja Manispaa ya Kibaha.


Nyongo amesema kuwa uzinduzi huo ambao una umuhimu mkubwa katika kuendeleza mfumo wa utambulisho wa wananchi na kuboresha matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma nchini na umuhimu wa watu kuelewa kuwa uzinduzi huo si tukio la kutambulisha kitambulisho kipya pekee bali ni hatua muhimu katika kuboresha mfumo wa utambulisho wa Taifa. 


"Mbali ya uzinduzi wa Kitambulisho cha Taifa Kilichoboreshwa toleo la 2026 NIDA pia atazindua rasmi huduma mpya inayojulikana kama "HUDUMA BILA FOLENI", inayolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma kupunguza muda wa wananchi kusubiri na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za Mamlaka hiyo,"amesema Nyongo.


Amesema huduma zitakazotolewa zitahusisha usajili wa wananchi ambao bado hawajajisajili katika mfumo wa NIDA uhakiki na marekebisho ya taarifa za utambulisho pale inapobidi ufuatiliaji wa hatua na hali ya maombi ya Vitambulisho vya Taifa.


"Utoaji wa Vitambulisho vya Taifa vilivyokamilika kwa wananchi wenye namba ya utambulisho wa Taifa (NIN) ambao bado hawajavichukua kutoa elimu na ushauri kuhusu taratibu na huduma mbalimbali zinazotolewa na NIDA.


Aidha amesema kuwa uzinduzi huo unatoa fursa ya kipekee kwa wananchi kupata taarifa kutatua changamoto zinazohusu utambulisho wao na kunufaika na huduma za NIDA bila kulazimika kusubiri fursa nyingine.


"Natoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Pwani

kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uzinduzi huo na kutumia fursa ya kupata huduma mbalimbali zitakazotolewa na NIDA na kumsikiliza Waziri Mkuu,"amesema Nyongo.


Katika hatua nyingine amesema Novemba 21 Waziri Mkuu atafanya ziara katika Halmashauri ya Chalinze ambapo atafanya Mkutano wa hadhara katika viwanja wa Polisi Chalinze.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UJUE UKWELI KUHUSU JIJI LA MBEYA (GREEN CITY)

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA

KAMISHNA DKT.BADRU ATUA KAMBI YA TIMU YA NGORONGORO KAMA SELEMANI MWALIMU

TIMU YA NGORONGORO KAMA DOUMBIA