RIDHIWANI AKEMEA UKABILA UKONGA

Na Richard Mwaikenda

MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete amekemea hisia  za ukabila zilizozuka na kuwagawa wananchi katika Jimbo Ukonga, Dar es Salaam.

Aliwaasa watu wanaoendekezatabia hiyo mbaya, alipokuwa akihutubia katika mkutano wa ndani wa kampeni ya kupanga mikakati ya ushindi wa kishindo kwa CCM, jana katika Kata ya Kivule.

"Siku za hivi karibuni kuna hisia mbaya za ukabila  zimejitokeza katika Wilaya ya Ilala, hasa Jimbo la Ukonga, ambapo kuna watu wanafanya kampezi za kuchaguana kwa kufuata makabila yao ya wakurya, wajaruo na wazaramo,"alisema Ridhiwani.

"Tabia hiyo inashangaza sana! Imetokea mnamchukia mgombea ubunge eti kwa sababu ya kabila lake. Jamani acheni tabia hiyo, kwani maendeleo hayaletwi kwa ukabila au anayetuongoza, bali yanaletwa na Ilani nzuri ya CCM," aliongeza kusema Ridhiwani.

Alitoa mfano wa Rais wa Awamu ya Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Baba wa Taifa hayati Julius Nyerere, kuwa angeendekeza ukabila kwa kupendelea wazanaki, nchi hii isingekuwa kama ilivyo sasa.

"Wakati wa uhai wake, Nyerere hakusita kukemea udini na ukabila kwa sababu ni sumu ya maendeleo, amani na utulivu, hivyo inatakiwa nasi tumenzi kwa kuyachukia mambo hayo," alisema. 

Alisema kuwa lililopo mbele yao ni kumtafuta mtu mwenye uwezo, ambaye atasimamia vizuri maendeleo ya jimbo hilo na kwamba kwa hivi sasa si mwingine bali ni mgombea wao ubunge Eugen Mwaiposa na madiwani.

Naye Mgombea ubunge wa Jimbo hilo, kupitia CCM, Mwaiposa, alishukuru kwa nasaha alizozitoa Ridhiwani na kwamba watajipanga kuzifanyia kazi ili CCM ishinde kwa kishindo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI