Meneja Masoko wa Precision Air,Emillian Rwejuna akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hotel ya Peacock,jijini Dar.
Peacock Hotel ni hoteli inayojali wateja wake kwa kiwango cha juu. Ili kudumisha na kuendeleza mila, desturi, na utamaduni wa mtanzania, hoteli ilianzisha Usiku wa Mtanzania ambapo vyakula vya asili ya Tanzania vinaandaliwa kwa ladha ya asilia. Ni hoteli pekee nchini Tanzania ambayo inadumisha menu halisi ya kitanzania.

Usiku huu unatimiza miaka kumi(10) mwaka huu tangu uanzishwe. Kila Jumatano usiku panakuwepo vyakula vya kitanzania vya aina mbalimbali na makabila mbalimbali. Mandhari ya hotel hugeuka kuwa ya asili ili kuleta maana halisi ya lengo la usiku huu.

Tarehe 3.12.2010 ni siku ya kusherehekea kutimiza miaka kumi ya Usiku wa Mtanzania katika ukumbi wa Karimjee kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 6:00 usiku.

Shamrashamra hizo zitapambwa na ngoma za asili pamoja na muziki kutoka kwa Kidum-Kenya, Lady Jay Dee, Sikinde-Ngoma ya Ukae, na Waane Star.

Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wateja wetu wote ambao wanaendelea kuburudika kwa milo ya kitanzania pamoja na burudani za asili. Kwa kutambua uwepo wao na kuthamini usiku huu tunawaahidi huduma bora zaidi na siku ya sherehe tutawatambua rasmi baadhi yao kwa niaba yaw engine kwa kuwapa zawadi.

Washiriki wenzetu katika kuunga mkono Usiku wa Mtanzania kutimiza miaka kumi ni Benki ya Posta, Shear Illussion, Vayle Springs, na Precision Air. Hawa wanadhihirisha dhamira yao ya kuunga mkono mila na desturi za kitanzania.
 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA