JK USO KWA USO NA RAIS GBAGBO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokelewa na Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo muda mfupi baada ya kuwasili jijini Abidjan kwa mazungumzo ya kutafuta suluhu na mpinzani wa Gbagbo Bwana Allasane Ouatarra. Rais Kikwete yupo katika jopo la kamati maalumu ya Viongozi wa Afrika walioteuliwa na Umoja wa Afrika(AU) kutafuta suluhu ya kisiasa nchini Ivory Coast.Viongozi wengine walio katika kamati hiyo ni pamoja na  Rais Jackob Zuma wa Afrika Kusini,Rais Idriss Deby wa Chad,Rais Blaise Compaore wa Burkina Fasso na Mwenyekiti wa kamati hiyo Rais Mohamed Ould Abdel Aziz wa Mauritania.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete(kushoto) pamoja na viongozi wengine akiwa katika mazungumzo na Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo(Kulia) katika ikulu ya nchi hiyo iliyopo Abidjan

Marais wanaounda kamati maalumu ya wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika katika kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa nchini Ivory Coast wakijadiliana jambo muda mfupi baada ya kukutana na kiongozi wa nchi hiyo Rais Laurent Gbagbo katika ikulu ya Abidjan jana jioni.Kutoka kushoto walioweka vichwa pamoja ni , Rais Idriss Deby wa Chad,Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini, Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa kamati hiyo Rais Mohamed Ould Abdel Aziz wa Mauritania(picha na Freddy Maro)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI