WAKENYA WATESA KILI MARATHON 2011

Mshindi wa mbio za umbali wa Km 42 Kipkemoi Kipsang wa Kenya  akimalizia mbio hizo  kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi katika mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro 2011.Alizawadiwa sh. miloni 3.(PICHA NA ZOTE RICHARD MWAIKENDA)

Mshindi wa kwanza wa mbio za umbali wa Km 42 kwa upande wa wanawake, Anna Kamau kutoka Kenya akimalizia mbio hizo  kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi katika mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro 2011.Alizawad iwa sh. miloni 3.(PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

Mshindi wa pili wa Km 42  kwa upande wa wananwake


Mwanamke mzee kuliko wote walioshiriki mbio za Km 5 za zilizoandaliwa na Vodacom katika mashindano ya Kilimanjaro, Eliansa Malisa akikabidhiwa zawadi na Mkuu wa Wilaya Hai, Dk Norman Sigala.


Waziri wa Habari Utamaduni Vijana na Michezo, Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimkabidhi mshindi wa kwanza wa Km 42, Anna Kamau zawadi ya sh. milioni 3 zilizotolewa na wadhamini wa Mashindano ya mbio za kimataifa za Kilimanjaro 2011, bia ya Kilimanjaro Premium Lager jana kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.


Mmoja wa  washiriki wa mashindano hayo akikimbia huku akiwa na bendera ya Taifa jana eneo la Mwika.


Mshindi wa kwanza wa mbio za Km 42,Kipkemoi Kipsang (kulia) wa Kenya  akichuana vikali na mkenya mwenzie Julius Kilimo muda mfupi kabla ya kumaliza mbio hizo. Kilimo alishinda nafasi ya pili.


Newar Twist akikimbia na mbwa wake,Barney Twist katika mashindano ya mbio za Km 21 katika mashindano ya kimataifa ya Kilimanjaro 2011, mjini Moshi leo.Yeye na mbwa wake walimaliza mbio ambapo hata mbwa alikabidhiwa medali na fulana vitu ambavyo kila mshiriki wa mashindano hayo alipatiwa.

wasanii wa kikundi cha Gifted Youth of Tanzania, Liner Juma na Ramadhan Mohammed wakicheza sarakasi wakati kikundi hicho kutoka Dar es Salaam kilipokuwa kikitumbuiza wakati wa mashindano hayo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI