BARCELONA MABINGWA ULAYA

Barcelona na kikombe baada ya mechi Wembley

Meneja wa Manchester United ya England, Sir Alex Ferguson, amekiri kwamba Barcelona ya Uhispania ndio timu bora zaidi ambayo timu yake imewahi kupambana nayo.

Ferguson amekiri hayo baada ya jana Man U kufungwa magoli 3-1, katika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.

Alisema kwamba vijana wake walipumbazwa na pasi za Barcelona, na kamwe hawakuweza kumzuia Messi, na baada ya Wayne Rooney kusawazisha katika kipindi cha kwanza, walitazamia wataweza kufanya vyema katika kipindi cha pili, lakini hayo hayakuwezekana.

Ushindi wa Klabu ya Barcelona ulisherehekewa sehemu mbali mbali duniani ambako mashabiki wa klabu hiyo waliburudika huku wale wa Manchester wakishindwa kuamini walichokishuhudia.

Kauli ya Kocha Mkuu wa Manchester United Sir Alex Ferguson kuwa Barcelona waliwaduwaza na kuwakubali kuwa Barcelona ni Timu Bora Duniani kwa sasa, iliungwa mkono na mashabiki wengi wa klabu hiyo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.