JK, MBOWE WASHIRIKI MAZISHI YA MAMAKE SPIKA MAKINDA


Naibu katibu mkuu wa Chadema Taifa Zitto Kabwe (kulia) akiteta jambo na katibu mkuu wa CCM Taifa Wilson MKama jana wakati wakisubiri Rais Jakaya Kikwete kuwasili kijiji cha Yakobi Njombe kwa ajili ya kuwawakilisha watanzania katika mazishi ya mama mzazi wa spika Anne Makinda. Picha Na Francis Godwin na Prosper Minja,Yakobi-Njombe-Bunge


Rais Jakaya Kikwete akichota mchanga tayari kwa kuuweka katika kaburi la marehemu Mama Tulakela Samnyuha, mama wa Spika wa Bunge, Anne Makinda wakati wa maziko ya mama huyo katika Kijiji cha Yakobi, wilayani Njombe mkoani Iringa. Katikati ni mke wa Rais, Mama Salma Kikwete






Msemaji mkuu wa kambi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa Taifa wa Chadema akiweka shada la maua katika kaburi la mama mzazi wa spika wa bunge Anne Makinda marehemu Tulakela Semnyuha aliyezikwa jana kijijini kwake Yakobi Njombe


Spika Makinda akiweka shada la maua kwenye kaburi la mama yake jana.





Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akijadili jambo na Kingozi wa Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe mara baada ya mazishi ya mama mzazi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika katika Kijiji cha Yakobi mkoani Njombe jana jioni.





Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI