MKE WA MUBARAK AKABIDHI MALI ZAKE MISRI



Hosni Mubarak na mkewe SuzanneMke wa rais aliyeondolewa madarakani wa Misri Hosni Mubarak, aliyekuwa akishikiliwa kwa makosa ya ulaji rushwa, ameachiwa kwa dhamana baada ya kukabidhi mali zake.
Maafisa walisema Suzanne Mubarak alikabidhi nyumba ya kifahari iliyopo kwenye kitongoji cha mjini Cairo na fedha zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 3 zilizoshikiliwa kwenye akaunti mbalimbali za benki nchini Misri.
Familia ya Bw Mubarak inakabiliwa na madai ya "kupata mali kinyume cha sheria" wakati alipokuwa madarakani kwa miaka 30.
Bw Mubarak aliyeondoshwa madarakani mwezi Februari pia anashutumiwa kuhusika katika mauaji ya waandamanaji waliopinga uongozi wake.
Watoto wake wawili wa kiume, Alaa na Gamal, kwa sasa wanashikiliwa kwenye gereza la Tora kwa makosa ya udanganyifu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.