OSAMA ALIVYOPIGWA RISASI


Osama bin Laden
Mwanzilishi na kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda, Osama Bin Laden, ameuwawa na majeshi ya Marekani nchini Pakistan, rais Obama amesema.
Kiongozi huyo wa al Qaeda aliuwawa baada ya makabiliano na wanajeshi wa Marekani nje ya mji wa Islamabad kwa mujibu wa taarifa za kijasusi.
Bw Obama amasema baada ya ufyatulianaji wa risasi, majeshi ya Marekani yaliuchukua mwili wake.
Bin Laden anashutumiwa kwa kuhusika katika baadhi ya vitendo vya ugaidi ikiwemo mashambulizi mjini New York na Washington, mnamo Septemba 11, 2001.
Kifo chake ni pigo kubwa kwa kundi la al Qaeda lakini kuna hofu kuwa huenda kukatokea mashambulio ya kulipiza kisasi.
Msako
Bw Obama amesema taarifa za mahali alikojificha zilianza kupatikana Agosti mwaka jana.
Kufuatia uchunguzi wa ujasusi waligundua amejificha mjini Pakistan.
Wiki iliyopita rais Obama alitoa amri kwa shughuli ya ''kumsaka bin Laden'' kufanyika. Bw Obama amesema operesheni hiyo iliendeshwa na kundi ndogo la wanajeshi wa Marekani katika eneo la Abbottabad, kaskazini mwa Islamabad.
''Baada ya ufyatulianaji wa risasi, bin Laden aliuwawa na mwili wale kuchukuliwa na majeshi ya Marekani'' rais Barack Obama amesema

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.