WAMISRI KUCHEZESHA SIMBA v WYDAD

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Misri
kuchezesha pambano la mkondo mmoja kati ya Simba ya Tanzania na Wydad Casablanca
ya Morocco litakalofanyika Mei 28 mwaka huu Uwanja wa Petrosport jijini Cairo,
Misri.


Mechi hiyo ya kutafuta timu ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa
Afrika itaanza saa 12 kamili jioni kwa saa za Cairo.


Waamuzi hao ni Farouk Mohamed atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake ni
Mohamed Waleed na Hassan Sherif. Mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Omar
Fahim wakati Kamishna wa mchezo huo ni Magdy Shams El Din kutoka Sudan.

Mshindi atacheza kundi B pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, Esperance ya
Tunisia na Moloudia Club d’Alger ya Algeria. Timu itakayoshindwa itaingia katika
hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo itacheza mechi ya
kwanza nyumbani dhidi ya Daring Club Motema Pembe ya DRC kati ya Juni 10, 11 na
12 mwaka huu.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Muhsin Balhabou ndiye atakayeongoza msafara wa timu ya Simba kwenda Cairo kwa
ajili ya mechi hiyo.

Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.