AAGIZA AZIKWE NA ALBAMU YA PICHA ZAKE

KIJANA Frank Raphael [18] amewaacha wazazi wake wakiwa na masikitiko makubwa baada ya kuamua kujinyonga kutokana kuwahurumia wazazi wake kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili na kuamua kujinyonga na kuacha ujumbe azikwe pamoja na picha zake alizopiga zilizopo kwenye album yake. Tukio hilo la kusikitisha limetokea huko katika Kata ya Isanga Mbeya mjini jana
Raphael alijinyonga kwa kutumia kamba aina ya katani kwa kile kilichodaiwa kuchoshwa na ugumu wa maisha unaowakabili wazazi wake kwa kumsomesha kwa shida ya hali ya juu na kuamua kufanya hivyo ili awaondolee mzigo wazazi wake hao
Kijana huyo mwaka jana alimaliza kidato cha nne na matokeo yake yalionyesha kuwa hakufanya vizuri na kipindi hiki alikuwa katika maandalizi ya kurudia mtihani huo
Hivyo kutokana na ugumu huo wa maisha unaowakabili wazazi wake ameamua kuwaondolea mzigo wazazi wake na kuacha ujumbe kwenye mfuko wake wa suruali aliyokuwa amevaa
“Naomba wazazi wangu wasituhumiwe kwa lolote.nimeamua kujinyonga mimi mwenyewe, naomba mnizike na picha zangu na madaftari niliyokuwa nikiyatumia shuleni” ulisema ujumbe huo wa kusikitisha
Frank ni mtoto wa kwanza kati ya watoto watatu katika familia yao, ameacha majonzi makubwa kwa wazazi wake kwa kitendo kilichofanywa na mtoto wao huyo kwani walisema wangekabiliana na ugumu wa maisha hadi mtoto wao aweze kumaliza shule.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.