DANIELA AMSHINDA VENUS KATIKA TENNIS

Daniela Hantuchova baada ya kujaribu kumshinda Venus Williams mara 11 hatimaye amshinda katika mashindano ya kimataifa ya tennis ya Aegon na kufuzu kwa nusu fainaliDaniela Hantuchova alifanya kazi ya ziada na baada ya kujaribu mara 11, hatimaye aliweza kumshinda Mmarekani Venus Williams katika robo fainali ya mashindano ya kimataifa ya Aegon, Eastbourne nchini Uingereza, na kufuzu kwa pambano la nusu fainali ya mashindano hayo ya tennis.
Hatuchova, kutoka Slovakia, ambaye alishikilia nafasi ya pili katika mashindano ya wiki iliyopita ya Aegon Classic mjini Birmingham, alianza vyema mashindano ya Alhamisi.
Alifanya kazi ya ziada na kumshinda Mmarekani Venus WillliamsMmarekani Williams alianza kuonyesha uhodari siku zake za kuwika katika tennis, huku upepo ukianza kuvuma mno.
Lakini Hantuchova alijitahidi na kujibu mashambulio yote, kiasi cha kuibuka mshindi kwa 6-2 5-7 6-2.
"Nahisi nilijitahidi na kucheza vyema mapema katika pambano hilo", alielezea mchezaji huyo anayeshikilia nafasi ya 29 katika orodha ya wachezaji bora duniani.
"Lakini upepo ulijitokeza kuyafanya mambo kuwa magumu kwa sisi wote wawili. Ikawa ni mchezo wa kiakili, na nilifuzu".
"Huu ndio wakati bora zaidi kwangu, msimu ya kuchezea katika nyasi, na ninahisi niko katika hali nzuri".
Hantuchova ilibidi afanye kazi ya ziada, hasa baada ya kushindwa kutumia hali ya kuongoza, akiwa na 4-2 katika mchezo, katika seti ya pili, na kumruhusu Williams kusawazisha, na kisha kulemewa 2-1 katika seti ya tatu, na kabla tu ya kupata ushindi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.