ETO'O ATAKIWA KUFIKA MBELE YA FECAFOOT

Mchezaji wa Inter Milan na timu ya taifa ya Cameroon Samuel Eto'o

Mshambulizi matata wa Inter Milan, Samuel Eto'o na wachezaji wengine wawili, watafikishwa mbele ya kamati ya nidhamu ya shirikisho la mchezo wa soka nchini Cameroon (Fecafoot).
Wachezaji hao wengine ni pamoja na Benoit Assou-Ekotto anayechezea klabu ya Tottenham na mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal, Alex Song.
Mashtaka dhidi yao yanahusiana na mechi yao ya kufuzu kwa fainali za kombe la taifa bingwa barani Afrika dhidi ya Senegal iliyochezwa tarehe 6 mwezi Juni mwaka huu na wakati walipokuwa kambini kabla ya mechi hiyo.
Eto'o ajitetea
"Ikiwa nimesababisha matatizo yanayohusu nidhamu katika kikosi chetu cha taifa, wana uhuru wa kuniadhibu," Eto'o aliliambia televisheni ya taifa nchini Cameroon.
Eto'o anahitajika kufika mbele ya kamati hiyo ya nidhamu kwa sababu hakushiriki katika mazoezi ya kikosi hicho, baada ya kutofautiana na Song na kuwa aliingilia kati mabadiliko ya wachezaji katika mechi yao dhidi ya Senegal.
Wakati wa mechi hiyo ambayo timu hizo mbili zilitoshana nguvu ya 0-0, Eto'o alielezea kutoridhishwa kwake baada ya mshambulizi Eric Maxim Choupo-Moting alipoondolewa na mahala pake kuchukuliwa na mlinda lango Henri Bedimo.
Song naye ameamrishwa kufika mbele ya kamati hiyo kufuatia majibizano yao na Eto'o.
mchezaji wa Arsenal Alex SongSiku chache kabla ya mechi hiyo, Song ambaye alikuwa akicheza mechi yake ya kwanza na kikosi hicho, kombe la dunia mwaka uliopita, alikataa kumsalimia Eto'o mbele ya vyombo vya habari na mashabiki wa timu hiyo ya taifa.
Assou-Ekotto naye anahitajika kuelezea sababu za kutofika kambini licha ya kuwa alifahamishwa mapema.
Wachezaji hao watatu wamepewa siku nane kujibu mashtaka dhidi yao na wana uhuru wa kufika mbele ya kamati hiyo wao wenyewe, au kutuma mawakili wao.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.