KIONGOZI WA ALQAEDA AFRIKA MASHARIKI AUAWA

Fazul Mohammed

Habari za kuuwawa kwa Fazul zinaongoza

Kuuwawa kwa kiongozi wa Al Qaeda katika Afrika Mashariki, Fazul Abdullah Mohammed, mjini Mogadishu Somalia, kumewafanya wakaazi wa kanda hiyo kupumua kidogo.
Fazul Abdullah Mohammed

Serikali ya mpito ya Somalia ilisema kuwa Fazul Mohammed aliuwawa kwa kupigwa risasi mapema juma hili, na ukaguzi wa DNA umethibitisha kuwa ni yeye.

Marekani imemshutumu kuwa alipanga mashambulio ya mwaka wa 1998 dhidi ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania, na kuuwa watu zaidi ya mia mbili.

Habari za kuuwawa kwa gaidi huyo zinaongoza Nairobi, na wakaazi kama Francis Ngina wana maoni yao:

"ikiwa yeye ndiye aliyepanga mashambulizi, inamaanisha washirika wake bado hawakupatikana.

Kwa hivo tukifikia shina la al-Qaida Afrika Mashariki, ndio tutaweza kuifyeka.

Na ndipo haki itatendeka kwa Wakenya 200 na watu wengine wa Afrika Mashariki kama Tanzania, ambao walikufa kwenye bomu wakati huo."

Wacha hawa watu waangamizwe.

Wanyonge walikufa hapa, kama mita 200 kutoka hapa nilipo.

Unakumbuka mwaka 1998 mwezi Agosti?

Naam, wacha hawa watu waangamie!"

Mdadisi wa maswala ya kisiasa na mwandishi wa habari Ahmed Rajab anasema" Si ajabu kuwa Fazul ameuwawa mjini Mogadishu, kwa sababu kwa muda mrefu akijulikana kuwa alikuwa kamanda wa kikundi cha wapiganaji wa Somalia, al Shabab.

Lakini tukumbuke kulikuwa na taarifa zamani kwamba aliuliwa na Marekani, na taarifa hizo zikawa si za kweli".

Kikundi cha al Shabab tayari kimetoa taarifa kusema kuwa Fazul Abdullah Mohammed hakuuwawa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.