,SIKUBALI SARAFU MOJA EAC; UJERUMANI

RAIS wa zamani wa Ujerumani, Profesa Horst Kohler ameonyesha wasiwasi na mpango wa haraka wa umoja sarafu unakusudiwa kutekelezwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC), ifikapo 2012.
Akizungumza katika hafla maalumu ya kuangalia matarajio na uhalisia wa EAC katika ulimwengu wa utandawazi mjini Arusha juzi, Profesa Kohler alisema kuharakisha mpango huo kunaweza kuleta mkanganyiko wa mambo siku zijazo kwani baadhi ya masuala yamsingi yanaweza kurukwa bila kujadiliwa na kupata makubaliano ya pamoja kwa maslahi ya wote.
“Kwanini haraka katika jambo la msingi na muhimu kama hili. Siamini na haiwezekani kutekeleza mpango wa kuwa na sarafu moja 2012 kama ilivyokubaliwa katika makubaliano ya EAC. Jambo hili lazima lijadiliwekwa makini na tahadhari kubwa,” alisema Profesa Kohler.
Aliwaambia wajumbe waliohudhuria hafla hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na Sekretarieti ya Afrika Mashariki na taasisi ya Kijerumani ya KonradAdenauer Stiftung kuwa baadhi mambo yanayohusu sarafu moja hugusa utaifa wa watu ambao uzoefu unaonyesha ni kitu muhimu kuliko vyote kwajamii yoyote.
Alitolea mfano wa mpango wa sarafu moja kwa nchi za Jumuiya ya Ulaya aliochukua muda wa zaidi ya miaka 10 tangu mwanzo wa mjadala ulioanza mwaka 1991 hadi mkataba uliposainiwa mwaka 1999 kabla ya utekelezajirasmi kuanza mwaka 2002 ulipozinduliwa sarafu na noti ya kwanza ya jumuiya hiyo (EURO)
“Kwa sababu hiyo, lazima yote yanayokusudiwa katika ushirikiano wa EAC upate kibali na uungwaji mkono kutoka kwa wananchi…ushirikiano usiwe mawazo na msukumo kutoka kwa viongozi wa kisiasa, lazimauzingatie mahitaji na maslahi ya wananchi,” alisema Rais huyo wa zamani.
Kuhusu mfumo wa soko huria, Rais huyo wa zamani ambaye jana alitembelea nchi ya Rwandaalisema lazima ziwepo sera na mfumo unaojali na kuzingatia faida na manufaa kwa wote msukumo mkubwa ukiwekwa katika maslahi ya jamii.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa EAC, Dk. Richard Sezibera alimhakikishia mgeni huyo nia thabiti ya kukamilisha na kutekeleza mipango yote inayokusudiwa katika ushirikiano wa nchi za ukanda huu wa Afrika Mashariki na kuongeza kuwa viongozi wote waliopo wameweka mbele nia na umuhimu wa mipango hiyo.
Dk Sezibera alisema pamoja na mambo mengine ushirikiano huo unapanua soko kubwa na la uhakika kwa bidhaa zinazozalishwa katika ukanda huo wenye jumla ya wakazi zaidi ya milioni 130 na tayari mipango yakuboresha miundombinu ya barabara, reli, anga na maji kurahisisha mawasiliano na kusarishaji wa watu na bidhaa za biashara umeanza kutekelezwa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.