TWIGA KWENDA ZIMBABWE

Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) inatarajia kuondoka Julai Mosi mwaka huu kwenda Harare, Zimbabwe kushiriki mashindano ya COSAFA yanayoanza Julai 2 mwaka huu jijini humo. Twiga Stars inayofundishwa na Kocha Charles Boniface akisaidiwa na Nasra Mohamed itaondoka saa 11 alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi ikiwa na msafara wa watu 26. Katika msafara huo wachezaji ni 19 huku benchi la ufundi likiwa watu wanne. Kiongozi wa msafara ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) Lina Mhando ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Twiga Stars inashiriki michuano hiyo ya Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA) ikiwa timu mwalikwa. Jumla ya timu nane zinashiriki wakiwemo wenyeji Zimbabwe. Nyingine ni Lesotho, Botswana, Afrika Kusini, Zambia, Msumbiji na Malawi. Twiga ambayo iko kundi A pamoja na Zimbabwe, Lesotho na Botswana itacheza mechi yake ya kwanza Julai 2 mwaka huu dhidi ya Botswana kwenye Uwanja wa Gwanzura.
Siku inayofuata itacheza na Lesotho kwenye Uwanja wa Rufaro kabla ya kumaliza mechi za makundi Julai 5 mwaka huu kwa mechi dhidi ya wenyeji kwenye Uwanja wa Gwanzura. Hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo itafanyika Julai 7 mwaka huu. Kila kundi linatoa timu mbili kuingia katika hatua hiyo na nusu fainali zote pamoja na fainali zitachezwa Uwanja wa Rufaro. Boniface WamburaOfisa Habari

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.