UGANDA YATOA BAJETI SH. TRILIONI 9

Rais Yoweri Museveni wa Uganda akiwa na Waziri wa Maji wa Tanzania alipowasili nchini kuhudhuria mkutano wa maendeleo ya uchumi Afrika Mei, Mwaka huu.

WAZIRI wa Fedha, Maria Kiwanuka amewasilisha bajeti inayofikia
Sh9.84 trilioni za Uganda, ambayo imeelekeza vipaumbele katika
miundombinu na huduma muhimu za jamii.
Vipaumbele katika mbajeti hiyo ni elimu, afya, barabara na sekta ya
nishati ambazo zimechukua zaidi ya nusu ya bajeti hiyo. Kiwanuka
alisema Sh6 trilioni ni mapato ya ndani na Sh3.3 trilioni ni mapato
kutoka kwa wahisani na wafadhili wa maendeleo.
Kipaumbele Kisekta Sekta ya elimu inaongoza kwa kupata mgao wa bajeti ya asilimia 15.5,
ikifuatiwa na sekta ya nishati na maendeleo ambayo imepata ongezeko la
mara tatu katika matumizi ya fedha zilizotengwa. Alisema Sh828.6 bilioni
zimetegwa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Karuma.
Sekta ya uwajibikaji, imetengewa asilimia 50 katika bajeti yake, ikiwa ni
ya pili baada ya ile ya nishati. Upande wa utawala wa umma bajeti yake,
imepunguzwa na kupoteza robo ya bajeti ya mwaka jana.
Ukuaji wa uchumi Alisema pato la bidhaa na huduma (GDP) lilipanda katika kipindi
kilichopita na kufikia asilimia 6.3 ikilinganishwa na asilimia 5.5 mwaka
wa fedha uliopita.
Hiyo ilichangiwa na ukuaji wa sekta ya kilimo na pia sekta ya mifugo
ambayo ilikuwa kwa asilimia 3.0 wakati uzalishaji wa chakula ulikuwa
kwa asilimia 7.5 ikilinganishwa na asilimia 6.5 katika mwaka wa fedha
uliopita.
Alisema sekta ya viwanda iliboreshwa na kukua kwa wastani wa asilimia
7.5 ikilinganishwa na asilimia 6.5 mwaka uliopita. Nchini Kenya,
WAZIRI wa Fedha wa Kenya, Uhuru Kenyatta amewasilisha bajeti yake
ya mwaka wa fedha wa 2011/12, ikilenga kuondoa mfumuko bei nchini
humo.
Bajeti hiyo inayofikia Dola 13.4 bilioni za Marekani imeelekeza
kupaumbele katika elimu, kilimo, afya na kukabiliana na mfumuko wa bei
hasa kutokana na ongezeko la mafuta na bei za bidhaa.
Kenyatta alisema Katika bajeti hiyo, serikali imetenga Sh100 bilioni za
Kenya kwa ajili ya kilimo kama sehemu kuelekea kufanya Kenya iwe na
chakula cha kutosha.
Kenyatta alisema Sh840 milioni za Kenya zimeelekezwa Wizara ya Elimu
kwa ajili ya kuwawezesha watoto wa masikini kwenda shule. Alisema
serikali imetenga Sh397 milioni kwa ajili ya maendeleo ya watoto wadogo
katika vituo mbalimbali.
Alisema Sh.54 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kununua dawa za
kupunguza makali ya Ukimwi (ARV) na vifaa vya kisasa kwa ajili ya
uchunguzi wa wagonjwa wa kansa ya kizazi.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.